Tuzo Za Muziki Zazinduliwa Rasmi Kwa Mwaka 2023

[Picha: Mwananchi]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Moja kati ya vitu ambavyo vinapamba muziki wa Tanzania ni tuzo na kwa mwaka huu wa 2023 tayari Baraza La Sanaa Tanzania maarufu kama BASATA wameshatangaza kwamba Tuzo Za Muziki maarufu kama Tanzania Music Awards zimerudi tena.

Uzinduzi huo wa kihistoria upifanyika siku ya jana Tarehe 14 Februari mwaka huu wa 2023 eneo la Warehouse Masaki ambapo baadhi ya wanamuziki na wadau wa muziki Tanzania walipata nafasi kuhudhuria huzinduzi huo  wa kihistoria.

Akizungumzia kuhusu tuzo hizo, Karibu Mtendaji Wa BASATA Dkt Kedmon Mapana amedokeza kuwa kwa mwaka huu wa 2023 vipengele vya tuzo vitaongezeka kutoka 10 mpaka 16 ambapo baadhi ya vipengele vilivyoongzeka ni pamoja na Mtangazaji bora muziki TV / Redio, Meneja Bora Wa Muziki pamoja na msanii bora wa Dancehall.

Aidha Mapana aliongeza kwa kusema kuwa kama mwaka jana ilivyokuwa, mwaka huu wasanii watatakiwa wajisajili na kuchagua wao vipengele ambavyo wanadhani wanastahili kuwania tuzo hizo.

Ikumbukwe kuwa kwa mwaka 2022 Ali Kiba aliongeza kwa kuchukua tuzo tano akifuatiwa na Harmonize, Nandy na Sholo Mwamba ambao walibeba tuzo 3.

Leave your comment