Ubashiri Mechi ya Bayern Munich Vs VFL Bochum -Mdundo Alt

[Picha:Bavarian Football Works]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Vinara wa ligi ya Bundesliga Bayern Munich wakiwa katika viwanja vyao vya Allianz wana kuwa wenyeji wa VFL Bochum katika mzunguko wa 20 wa ligi hiyo.

Bayern Wana nafasi zaidi ya kubeba mkononi alama tatu mara baada ya kushinda michezo minne kati ya mitano waliyokutana  hapo awali huku bayern pia wakiwa na ushindi mkubwa katika baadhi ya mechi.

Licha ya kuwa na majeruhi Bado Bayern Munich wamezidi kubaki kileleni katika ligi, na sasa wamekamilisha dirisha dogo la usajili mwezi Januari baada ya kuongeza nguvu na kusajili wachezaji kama Joao cancelo kwa mkopo pamoja na Yann Sommer.

Wakiwa nafasi ya 15 na alama 19 Bado Bochum wanahitaji nguvu zaidi haswa mbele ya kikosi chenye nguvu kama Bayern Munich.

Majeruhi ni wengi kwa viongozi wa ligi lakini licha ya yote wamejizatiti na kujihakikishia wamebaki katika nafasi ya kwanza ukilinganisha na VFL Bochum ambao wana majeruhi wawili pekee ambao ni Michael Esser pamoja na Cristian Gamboa

Odds za Bayern Munich kushinda mchezo huu ni 1.12

Leave your comment