Hatimaye Simba yakamilisha uchaguzi - Mwenyekiti na wajumbe -Mdundo Alt

[Picha:Pintrest]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu ya soka ya Simba hatimaye imefanikiwa kumpata Mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya kukamilisha uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere International Convertion Center (JNICC)

Baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika katika uchaguzi huo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Boniface Lihamwike alimtangaza Murtaza Mangungu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Wekundu wa Msimbazi kwa jumla ya kura 1311 akimpiku mpinzani wake Moses Kaluwa aliyepata jumla ya kura 1045.

Pia Mwenyekiti wa uchaguzi aliwataja wajumbe walioshinda katika nafasi hizo ambao ni pamoja na Dr. Seif Ramadhan Muba, Asha Baraka, CPA Issa Masoud Iddi, Rodney Chiduo pamoja na Seleman Hatubu.

Klaba ya uchaguzi kuanza Mwenyekiti huyo aliihakikishia Klabu ya Simba na wanachama wake ya kuwa wataanza kufungua ukurasa mpya kwa ajili ya maendeleo ya Simba.

Pia mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makala amewapongeza wanasimba kwa mafanikio waliyonayo na haswa kwa kutimiza zoezi hilo la kupiga kura.

Leave your comment