Newcastle Yaipiku Chelsea Kumsajili Anthony Gordon -Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Wakati Everton ikiwa bado inatapatapa ikijikongoja kutokushuka daraja hatimaye Newcastle United wamefanikiwa kumsajili winga wa timu hiyo Anthony Gordon kwa kitita cha Euro milioni 40.

Masaa machache Newcastle walithibitisha kuwapiku Chelsea walipokuwa nao mezani kumuwania Gordon baada ya Newcastle kuthibitisha hilo kupitia mitandao Yao ya kijamii.

Winga huyo baada ya kukamilisha usajili wake na kwenda katika viunga vya Saints James' Park amewaacha mashabiki wa Everton na waraka mrefu katika ukurasa wake wa Instagram.

Katika waraka huo baadhi ya aliyoyaandika ni pamoja na  "Naipenda hii klabu na siku zote itakuwa hivyo tangu siku nilipojiunga lakini umefika muda wa Mimi wa kuondoka. Najua wengi hamtanielewa lakini sura mpya inanisubiri. Siku zote nitakuwa nikiitakia klabu hii mema na siku zote nitakuwa nikiiangalia"

Gordon alijiunga na Everton tangu alipokuwa na umri wa miaka 11 na kwa sasa huu ndio muda wake Sahihi wa kuachana na timu hiyo iliyomlea na kumkuza kwa zaidi ya miaka 10.

Wakati haya yote yanajiri Everton nao wako mbioni kumwajiri kocha wao mpya na huenda akawa Sean Dyche baada ya kumfuta kazi Lampard siku chache zilizopita.

Pia kwa Chelsea usajili huu umekuwa mwiba mchungu kwao kwani pia walikuwa wakimuwinda mchezaji huyo huku nao Benfica wakiendelea kumgomea Enzo Fernandez kwenda Stamford bridge licha ya The blues kupandisha dau.

 

Leave your comment