Al hilal Yatia Kambi Dar es salaam- Mdundo Alt

[Picha: Goal.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu ya soka ya nchini Sudan, Al Hilal imewasili jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano kwa lengo la kuweka kambi kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa Afrika katika hatua ya makundi itakayoanza mwezi Februari.

Ujio wa timu hiyo ni kutokana na kuwepo kwa ushirikiano kati ya klabu ya AL hilal dhidi ya klabu ya Simba mara baada ya kuingia mkataba wa mahusiano na mashirikiano huku kukiwa na maeneo saba yaliyohusisha mkataba huo.

Kabla ya kucheza na Simba katika mchezo wa mwisho wa kirafiki katika uwanja wa Benjamin Mkapa Al Hilal wataanza mechi za awali na mchezo wao wa kwanza wataucheza dhidi ya Namungo Fc huku ikifuata mechi yao dhidi ya wanalambalamba Azam Fc na michezo yote hii itachezwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Al Hilal iko katika kundi B ligi ya mabingwa Afrika na timu ambazo itakutana nazo ni pamoja na AL Ahly ya Misri, Mamelodi Sundown ya Afrika ya kusini pamoja na Coton Sport kutokea Cameroon.

Kwa upande wa Simba wao watakutana na klabu kama vile Vipers ya nchini Uganda, Horoya kutokea Guinea pamoja na Raja Club Athletic ya huko Morocco katika kundi C michuano ya mabingwa Afrika.

Leave your comment