Chelsea, Newcastle Mbioni Kumuwinda Anthony Gordon -Mdundo Alt

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu za Chelsea pamoja na Newcastle wako mbioni kuisaka saini ya winga kutokea Everton Anthony Gordon ambaye amebakiza takribani miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo.

Majira ya joto katika dirisha kubwa la usajili mwaka jana, Chelsea wakiwa chini ya Thomas Tuchel walishindwa kufanikisha usajili wa nyota huyo wa soka mwenye miaka 21 ambaye pia ni zao la Everton.

Katika kuipambania saini ya winga huyo Chelsea wako tayari kumuachia mchezaji wao Hakim Ziyech ili kuliziba pengo la Gordon Everton. Pia The Blues wako tayari kumuacha Anthony amalizie msimu huu na The Toffees ili kuisaidia isishuke daraja na kumsajili katika msimu ujao.

Kwa upande wao Newcastle wao hawako tayari mchezaji huyo abaki Everton kwani wako tayari kufanikisha usajili wake ili ajiunge na timu hiyo muda wowote watakapo kamilisha taratibu zinazostahili.

Klabu ya Everton imependekeza dau  la Euro Milioni 55 kutolewa kwa timu ya Chelsea au Newcastle ili waweze kuipata huduma ya mchezaji huyo. Lakini Newcastle wako tayari kutoa nusu ya pendekezo hilo.

Kwa msimu huu Anthony amefanikiwa kuweka kambani mabao matatu pekee huku akiwa hana pasi yoyote ya usaidizi wa goli.

Leave your comment