Ubashiri Mechi Ya Singida Big Stars Vs Azam Fc - Mdundo Alt

[Picha: Azam Fc]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mzunguko wa 21 unaendelea siku ya Jumatatu ambapo Singida Big Stars watakapo kuwa wenyeji kwa Azam Fc  katika ligi kuu ya Tanzania.

Katika mzunguko huu Azam wanaingia kifua mbele wakiwa nafasi moja juu ya Singida huku pia wakiwa tayari wamesha mfunga katika mechi yao ya kwanza walipokutana mwezi Octoba kwa Azam kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Licha ya kuwa hii ndiyo mara yao ya kwanza kushiriki  ligi kuu lakini Singida wamethibitisha kuwa ni moja ya timu zenye upinzani kwa sasa wakiwa nafasi ya nne huku wakifika fainali katika kombe la Mapinduzi waliposhindwa kung’ara mbele ya Mlandege.

Wanalambalaba wakiwa katika nafasi ya tatu katika msimu huu kwa sasa wanazidi kuwa mwiba kwa wapinzani na katika michezo yao mitano ya mwisho waliyoicheza wamefanikiwa kushinda mechi 2, sare mechi 2 na kufungwa mechi 1.

Kwa upande wao Singida katika michezo yao mitano ya mwisho kuushiriki katika ligi wamefanikiwa kushinda michezo minne huku wakitoa ssare mchezo mmoja.

Huu ni moja kati ya ile michezo ya afe kipa afe beki kwa maana  ni mechi ya kutata na shoka hivyo odds kwa magoli kuwa chini ya 2.5 ni  1.58.

Leave your comment