Ali Kamwe ampongeza Metacha Mnata - Mdundo Alt

[Picha: Bongo5.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya klabu ya soka ya Yanga kufanya usajili wa mlinda mlango Metacha Mnata Afisa habari wa klabu hiyo Ali kwamwe amempongeza mchezaji huyo baada ya kuwataka radhi mashabiki wa Yanga kutokana na tukio la kuwavunjia heshima na kuondoka katika klabu hiyo akiwa amebeba chuki kwa mashabiki kutokana na tukio hilo.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Azamtvsports Ali Kamwe alisema ya kuwa "….kama Kuna mahala amewahi (Metacha) zungumza kama alivyozungumza kwenye hiyo clip alivyozungumza akiomba msamaha mashabiki wa Young Africans, ame-post kwenye page yake akiomba radhi na akikiri kutambua kwamba alikosea ….."

Masaa machache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa klabu ya Yanga iliingia sokoni kumtafuta mlinda mlango kwa haraka baada ya golikipa Aboutwalib Mshery kuwa na majeraha yatakayomkalisha nje ya Uwanja kwa muda mrefu.

Usiku huohuo Metacha akapatikana na kujiunga na Yanga kwa mkopo akitokea Singida Big Stars kwa mkataba wa miezi sita.

Afisa habari huyo pia aliupongeza uongozi wa Yanga akiwemo Rais wa klabu hiyo Hersi Ally Said pamoja na makamu wake Arafat Haji kwa kuweka maslahi ya Yanga mbele kuliko kitu chochote.

Leave your comment