Ubashiri Mechi ya PSG Vs Al Nassr, Al hilal - Mdundo Alt

[Picha: Tribun]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Vigongo wa soka Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo wanakutana uso kwa uso katika uwanja wa King Fahd International stadium baada ya miaka kadhaa kupita tangu watunishuane misuli. Mchezo huo utachezwa siku ya Alhamis huko Saudi Arabia katika Jiji la Riyadh.

Uwanja wa King Fahd wenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 60,000 ndicho kiwanja ambacho pia kilihusika katika fainali za Super Cup na Barcelona kuibuka washindi siku ya Jumapili.

Katika mchezo huu PSG ya Ufaransa watafunga safari katika mchezo wa kirafiki utakao wakutanisha dhidi ya muunganiko wa timu mbili Al Nassr anayotoka Ronaldo pamoja na Al hilal ukiwa ni mchezo wa kirafiki, huku muunganiko huo ukipewa jina la timu ya msimu ya Riyadh.

Majeruhi wa uhakika kwa Paris Saint Germain ni mfaransa Presnel Kimpembe, muitaliano Marco Verratti, pamoja na beki wa kireno Nuno Mendes.

Kwa upande wa kikosi cha msimu cha Riyadh watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo wakiwa hawana majeruhi yoyote.

Cristiano Ronaldo ndiye atakayevaa kitambaa cha unahodha katika mchezo huo baada ya kukabidhiwa dhamani hiyo ya kuongoza kikosi hicho cha Riyadh.

Baada ya mchezo huu kiu ya mashabiki ya kuwashuhudia kwa pamoja nyota Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo itakuwa imepungua kama siyo kukatika kabisa. Odds za timu zote mbili kupata magoli ni 1.71

Leave your comment