Ripoti Mechi ya Barcelona Vs Real Madrid-Fainali Super Cup - Mdundo Alt

[Picha:FC Barcelona]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu ya soka ya nchini Uhispania Barcelona imempatia kichapo Real Madrid Cha mabao 3-1 katika fainali za Super Cup zilizochezwa katika uwanja wa King Fahd International stadium siku ya Jumapili.

Katika mchezo huo Barcelona wakiwa na kocha wao Xavi Hernandez walifanikiwa kupata matokeo mapema ambapo mabao Yao mawili yalipatikana katika kipindi Cha kwanza no kutoka kwa mhispania Gavi baada ya kusogezewa pasi ya usaidizi wa goli kutoka kwa straika Robert Lewandowski.

Bao la pili pia lilisababishwa na wahusika wa bao la kwanza mara baada ya Lewandowski kupatiwa pasi ya usaidizi wa goli kutoka Gavi na Lewandowski kutikisa nyavu za Los Blanco.

Katika kipindi Cha pili dakika ya 69 Pedri naye akakamilisha bao la ushindi kwa Barca.

Fainali hizi zimempa majonzi Carlo Ancelotti na kikosi chake katika dabi hii ya El Clasico kwa kushindwa kunyakua kombe hilo la Super cup. Bao la kufutia machozi kwa Madrid walilipata kupitia kwa straika wao Karim Benzema katika zile dakika za nyongeza.

Barcelona walionekana kuutawala mchezo wakiwa na nguvu ukilinganisha na Real Madrid ambao wao walikuwa wakicheza kwa mashaka ambayo yalipelekea kupoteza mchezo huo.

Kinda Pablo Martín Gavira ndiye mchezaji Bora wa mchezo na ukali wake huo anaendelea kuunogeshea naksi akiwa na Miaka 18 pekee.

Leave your comment