Ubashiri mechi ya Yanga Vs Ihefu -Mdundo Alt

[Picha:Goal.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu ya soka ya nchini Tanzania, Young Africans sport club inatarajiwa kukutana na Ihefu siku ya Jumatatu katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga kwa sasa wakiwa vinara wa ligi kuu nchini Tanzania mara ya mwisho kukutana na Ihefu waliambulia kipigo Cha bao 2-1 na kuwafanya wavunje mwiko wa Unbeaten kwa zaidi ya mechi 40.

Ihefu yenye maskani yake jijini Mbeya inaingia katika mchezo huo ikiwa nafasi ya 13 huku mchezo wao wa mwisho wakibeba alama tatu mara baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya KMC.

Katika mchezo huu Feisal Salum huenda akakosa kushiriki na kikosi Cha Yanga kutokana na muendelezo wa sakata lake na timu hiyo licha ya shirikisho la soka Tanzania kumtambua kama mchezaji wa Yanga.

Ihefu ikiwa chini ya Mwalimu Zuber Katwila amekua tishio kwa Yanga mara baada ya mabeki wa timu hiyo kusifiwa katika mchezo wa hapo awali timu hizi mbili zilipokutana.

Straika Fiston Mayele anatazamiwa kuwatetema Wana Yanga na kwa sasa akiwa na jumla ya mabao 14 na kuwa kinara wa mabao ligi kuu Tanzania bara.

Huu ni mchezo wa kisasi kwa Yanga huku nao Ihefu wakihitaji alama zaidi ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi katika ligi kuu.Odd za Yanga kupata alama tatu ni 1.55

Leave your comment