Joao Felix Aanza Vibaya na Chelsea -Mdundo Alt

[Picha:Surprise Sports]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Nyota wa soka anayekipiga katika klabu ya Chelsea kwa sasa Joao Felix ameanza vibaya na timu hiyo mara baada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kupewa kadi Nyekundu kutokana na kumfanyia madhambi mchezaji wa Fulham Kenny Tete wakati alipojaribu kumkaba katika dakika ya 58.

Katika mchezo huo ambao Chelsea walikuwa katika uwanja wa ugenini walishuhudiwa wakipata kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya kikosi cha Marco Silva ambacho kimepanda daraja msimu huku.

Baada ya mchezo kukamilika kocha wa Chelsea Graham Potter wakati wa mahojiano baada ya mchezo huo aliitaja kadi aliyopewa Joao Felix kuwa ni moja ya sababu zilizoifanya Chelsea kupoteza mchezo huo dhidi ya Fulham.

Kabla ya kutua The blues Joao Felix alitajwa kuwa na uhusiano mbaya na kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone ndipo Chelsea wakaamua kuitumia nafasi hiyo kuinyaka Sahihi ya mchezaji huyo kwa mkopo.

Mbali na Joao Felix pia Chelsea katika dirisha hili dogo wamefanikiwa kuwasajili wachezaji kama vile David Datro Fofana pamoja na Benoito Badiashile.

 

Leave your comment