Ubashiri Mechi ya Manchester United Vs Manchester City -Mdundo Alt

[Picha:Surprise Sports]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Manchester United wanavaana na Manchester City katika mchezo utakaochezwa uwanja wa Old Trafford siku ya Jumamosi.

Mahasimu Hawa wa kihistoria hii ni mara Yao ya pili kukutana katika msimu huu mara baada ya  City kummwagia karamu ya mabao 6-3 Manchester United Katika mechi Yao ya kwanza mechi iliyochezwa mwezi Octoba City walipokuwa wenyeji.

Katika mchezo huo straika Erling Halaand pamoja na Phil foden walifanikiwa kupata hat-trick na kurahisi mchezo wao dhidi ya mashetani wekundu.

Baada ya kuwepo kwa mapungufu katika upande wa straika katika kikosi Cha Erik Ten Hag hatimaye wamefanikiwa kumsajili straika Wout Weghorst kutokea klabu ya Beşiktaş kwa mkopo na huenda akaongeza nguvu katika safu ya mashambulizi kwa United.

Bado Jadon Sancho atakuwa nje ya Uwanja huku pia naye Don Van de Beek akikosa mchezo huo pamoja na majeruhi wengine akiwemo Diego Dalot aliyepata majeraha katika mchezo wa United dhidi ya Charlton Athletic.

Majeruhi wengine ni pamoja na Axel Tuanzebe pamoja na Phil Jones.

Pep Guardiola kwa upande wake majeruhi ni mmoja mpaka sasa ambaye ni beki wa kati kutokea Ureno Ruben Dias akiwa na majeraha ya paja.

Manchester City wanaweza kuwa katika hali Bora zaidi kuliko United lakini pia United wamerejea vyema baada ya kombe la Dunia huku Rashford naye akionesha kuzidisha makali uwanjani.

Kama ilivyo ada mechi za dabi ni kati ya michezo ambayo matokeo yake ni magumu kuamuliwa kabla ya mchezo hivyo basi Odds kwa magoli kuwa zaidi ya mawili ni 1.22

Leave your comment