Uchambuzi Wimbo 'Assalaam' Wa Mbosso ft Mohammed Almanji -Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Moja kwa moja mpaka Oman, Mbosso anatukutanisha katika kolabo yake na msanii mashuhuri wa nchi hiyo Mohammed Almanji katika wimbo uliopewa jina la Assalaam ambao ni wimbo namba tano katika Extended playlist yake ya kwanza ya kuitwa Khan.

Msanii huyo kutokea lebo ya WCB Wasafi ni moja kati ya wasani ambao wamekuwa wakisifika kwa uandishi wa nyimbo za mahaba ambazo zimekuwa zikiburudisha zaidi na kupendwa na kumfanya hata kubadilishwa kwa jina lake kutokea Mboisso mpaka kuitwa Mbosso Khan jina hili akipewa kutoka kwa muigizaji kutokea nchi ya India Sharuk Khan.

Assalaam ni neno la kiarabu ambalo lina asili yake katoka nchi zenye asili ya kiarabu linalotumika katika salamu baina ya watu. Mbosso katika wimbo huo amepata nafasi ya kuelezea jinsi ambavyo amemkubuka mpenzi wake na kutokana na umbali imemfanya apate maumivu.

Kutokana na mapenzi yake juu ya utamaduni wa bara la Asia, Mbosso katika kolabo yake hii ameweza kupita vizuri katika wimbo huo ukiwa na na ladha murua kabisa ya Bongo Fleva huku pia ukipita katika maadhi maridhawa ya kiarabu na kunogesha zaidi wimbo huo baadaya Mohammed Almanji kupita katika lugha ya kiarabu.

Kutokea lebo moja na Mbosso producer kutokea Wasafi WCB Lizer Classic ndiye aliyeuandaa wimbo huo ambaye pia katika EP hiyo amehusika katika nyimbo kama vile Huyu hapa pamoja na Yataniua ambazo zote amezifanyia Mixing.

https://www.youtube.com/watch?v=7giiq_OgV_Y

Leave your comment