Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Sadio Mane Kukosa Kombe La Dunia- Mdundo Alt
18 November 2022

[Picha:Instagram]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Taarifa za kusikitisha simejiri mara baada ya Senegal kumkosa mshambuliaji wao Sadio Mane kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata wiki iliyopita wakati Bayern Munich walipokuwa wakicheza na Werder Bremen.
Taarifa hizi zimejiri mara baada ya Mane kukamilisha upasuaji wa goti lililopata majeraha na kuonekana ya kuwa bado hatoweza kushiriki kombe la dunia.
Shirikisho la soka nchini Senegal lilitangaza ya kuwa Mane hatoshiriki mechi za mwanzo za kombe la dunia kutokana na majeraha lakini pia watamtibu kwa kutumia miti shamba jambo ambalo limeonekama kushindikana.
Kwa kocha wa Senegal Aliou Cisse atalazimuka kuziba pengo hilo ambali pia ni pigo kwa kikosi kizima cha Senegal na mzibaji wa nafasi hiyo anaweza kuwa mshambuliaji kutokea Watford Ismaila Sarr.
Siku ya Jumatatu Senegal watacheza dhidi ya Netherlands kabla ya kuvaana na wenyeji wao Qatar na kukamilisha kwa kukichapa dhidi ya Ecuador katika kundi A.
Weekly Top 10 songs

Inama4:58
ONLY YOU JESUS5:44
Bikyaganye3:29
Mshamba2:44
Daddy2:50
Come Alive3:32
Sissa3:37
Alaska2:29
Deep House BLACK5:35
Eazzy Ft Way Dee2:59
Top stories
- My incoming songs
09 October
- HOTKEED BIOGRAPHY, CAREERS AND AWARDS.
09 October
- LK GRECK BIO DATA
10 October



Leave your comment