Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Nkunku Na Majeraha Ya Goti Kuelekea Kombe La Dunia
16 November 2022

[Picha:Instagram]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Habari za kusikitisha zimejiri katika timu ya Taifa ya Ufaransa mara baada ya Christopher Nkunku kupata majeraha ya goti wakati alipokuwa akifanya mazoezi na timu hiyo.
Majeraha hayo ya goti yamejiri zikiwa zimebaki siku tano pekee kombe la dunia kuanza kutimua vumbi huko nchini Qatar.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 25 ambaye pia anakipiga huko RB Lepzig atakosa kushiriki kombe na dunia kutokana na majeraha hayo ikiwa hii ndiyo mara yake ya kwanza kushiriki kombe la dunia.
Ufaransa tayari wameshathibitisha majeraha hayo na pia inasemekana ya kuwa Randal Kolo Muani kutokea Einchracht Frankfurt ndiye ataichukua nafasi hiyo ya Nkunku.
Wakati hayo yanajiri Chelsea wanasemekana nao wanakamilisha mazungumzo ya kumsajili Nkunku katika msimu ujao na ya kuwa mazungumzo yako katika hali nzuri.
Weekly Top 10 songs

Inama4:58
ONLY YOU JESUS5:44
Bikyaganye3:29
Mshamba2:44
Daddy2:50
Come Alive3:32
Sissa3:37
Alaska2:29
Deep House BLACK5:35
Eazzy Ft Way Dee2:59
Top stories
- My incoming songs
09 October
- HOTKEED BIOGRAPHY, CAREERS AND AWARDS.
09 October
- LK GRECK BIO DATA
10 October



Leave your comment