Cristiano Ronaldo Aiwakia Manchester United- Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Nyota wa soka mwenye asili ya Ureno na anayechezea timu ya Manchester united Cristiano Ronaldo hatimaye amevunja ukimya juu ya hisia zake ndani ya United wakati alipofanya mahojiano ya moja kwa moja na mtangazaji wa Talktv Piers Morgan.

Katika mahojiano hayo mshindi huyo wa tuzo tano za Ballon d'or alieleza ya kuwa anajisikia kusalitiwa ndani ya United na kuwa wapo watu wanaomlazimisha kuondoka katika klabu hiyo mashuhuri ya soka duniani.

Ronaldo aliwataja watu mbalimbali akiwemo kocha  aliyepita wa klabu hiyo Ralf Rangnick na kusema ya kuwa hata hakuwa akimfahamu huku akieleza ya kuwa kwa kocha wa sasa Erik Ten Hag ya kuwa hawezi kuonesha heshima kwake kutokana na kocha huyo kumvunjia heshima.

Pia nguli huyo wa soka hakumuacha salama Wayne Rooney juu ya madongo anayomtupiaga na kusema '... siwezi kusema mimi ni mzuri zaidi yake. Ambao huo ndio ukweli…'

Ronaldo na Rooney walishawahi kucheza pamoja Manchester United miaka ya hapo nyuma lakini kwa sasa Rooney ni kocha.

Sakata hili limezuka siku chache kuelekea kombe la dunia na miezi michache pia imepita tangu tetezi za mshambuliaji huyo ziibuke za kutaka kuondoka klabuni hapo.

Leave your comment