World Cup Team Review : Kurunzi kwa Costa Rica Group E- Mdundo Alt

[Picha:Goal.com]

Mwandishi: Peter Pinchez

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Costa Rica watakuwa wakishiriki kombe la dunia kwa mara ya 6 sasa, hii ikiwa ni ya tatu mtawalia.Kikosi hiki kinachofunzwa na kocha Luis Fernarndo Suarez kitajaribu kuzifufua kumbukumbu za kombe la dunia la 2014. Walipomaliza kileleni mwa kundi wakiondolewa kwenye robo fainali na Uholanzi watakapokabiliana na mabingwa wa 2010 Uhispania wanaoshiriki kombe la duni kwa mara ya 16, Ujerumani ambao ni mabingwa mara nne wa dunia na Japan vigogo wa asia.

Kwenye orodha ya Fifa Costa Rica inaorodheshwa ya 31, nafasi ya 13 ikiwa ndiyo nafasi nzuri kwao kuwahi orordheshwa na fifa,mwaka wa 2015.Japo ukilinganisha vikosi ,uzoefu nafasi za Costa Rica kutinga raundi ya 16 ni finyu japo makubwa hufanyika kwenye kombe la dunia.

Mlinda lango wa timu ya PSG Keyler Navas ana uzoefu kwenye kikosi akisakata mechi 107 sawa na nahodha bryan ruiz aliyeisakatia mechi 144.

Leave your comment