FKF Yafuta Ligi Ya 2021/22

[Picha: Hon. Ababu Namwamba /Twitter]

Mwandishi: Peter Pinchez

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Shirikisho linalosimamia soka nchini fkf kupitia kwa mkurugenzi wake barry otieno limetoa taarifa likifutili mbali ligi ya msimu wa 2021/22 ya FKF Premier League, NSL, FKF division 1 na FKF women premier league zilizoendeshwa na kamati ya muda iliyoteuliwa na waziri wa zamani Amina Mohammed.

Kulingana na taarifa hii hamna timu itakayo shushwa wala kupandishwa daraja kwenye ligi hizi. Vile vile, FKF itafuata matokeo ya ligi ya division 2 na zile za maeneo zilizoendeshwa na usimamizi wa FKF kwenye maeneo hayo.

FKF pia imetangaza kuwa msimu moja wa ligi kuu utang’oa nanga mnamo Novemba 19 huku ligi kuu ya kina dada iking’oa nanga Novemba 26.

Leave your comment