Majeruhi Brazil Kuelekea Kombe La Dunia

[Picha: Premier League]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kuelekea kombe la dunia lililobakiza siku chache kuanza huko Qatar, timu ya taifa ya Brazil ambao pia ni washindi wa kombe hilo mara tano dunia, Brazil wamepata pigo kwa kuwa na majeruhi katika kikosi chao ambao wanawafanya wakose moja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho cha timu ya Taifa.

Moja kati ya majeruhi ni mshambuliaji anayekipiga huko Tottenham hotspurs Richarlison ambaye aliripotiwa kuumia  wakati Spurs walipokuwa wakicheza na Everton. Ripoti kutoka kwa kocha wa Spurs Antonio Conte amesema ya kuwa mchezaji huyo atakuwa tayari kushiriki kombe la dunia kwani majeraha hayo yatakuwa sawa kwa wakati huo.

Majeruhi mwengine ni kiungo Arthur Melo kiungo kutokea Juventus anayekipiga huko Liverpool ya Uingereza kwa mkopo. Mchezaji huyo ameripotiwa kukosa mashindano hayo na kuwa majeraha hayo ya paja ni majeraha ya muda mrefu na yatamgharimu kushiriki kombe hilo la dunia nchini Qatar.

Timu ya taifa ya Brazili kwa miaka ya nyuma imekuwa na sifa ya kuwa na wachezaji maarufu na mafundi katika soka duniani kama vile Ronaldo lakini pia kwa sasa timu hiyo pia inawachezaji mashughuri kama vile Neymar Jr wa PSG Vinicius Jr wa Real Madrid Gabriel Jesus wa Arsenal, Antony wa Manchester United pamoja na wengine wengi

Brazil ni moja kati ya timu ambazo katika kombe hili la dunia wataangaliwa kwa jicho la upeekee kutokana na uwezo wao pamoja na ushindani wa miaka nenda rudi katika mashindano haya makubwa ya kombe la dunia.

 

Leave your comment