Fahamu Upekee Wa Kombe la Dunia 2018

[Picha: CGTN]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kombe la dunia la mwaka 2018 ni mashindano yaliyoanza mwezi Juni tarehe 14 na kutamatika mwezi wa Julai 15 ambapo Ufaransa walishuhudiwa wakiibuka washindi wa mashindano hayo katika fainali zilizomkutanisha na Kroashia katika uwanja wa Luzhniki  na kuibuka na ushindi wa mabao nanne kwa mawili. Ushindi huo ni wa pili kwa Ufaransa katika ushiriki wao wa kombe la dunia baada ya miaka ishirini kupita tangu wapate ushindi wa kwanza wa kombe la dunia mnamo mwaka 1998.

Katika kombe hilo la dunia lililofanyika Urusi kuna baadhi ya mambo ambayo yalifanya mashindano hayo yawe ya kipekee zaidi ukilinganisha na mashindano mengine ya kombe la dunia, na mambo hayo ni kama yafuatayo.

Rekodi Ya Gharama Za Uandaaji

Urusi ilivunja rekodi katika gharama za uandaaji wa kombe la dunia la mwaka 2018 baada ya kutumia kiasi cha zaidi ya dola za kimarekami milioni kumi na moja na kuwa kombe la dunia la kwanza kuandaliwa kwa gharama kubwa zaidi. Gharama hizo zilijumuisha urekebishaji wa viwanja vya soka, hoteli pamoja na ujenzi wa barabara na vituo vikuu vya polisi. Kwa sasa Qatar inakwenda kuvunja rekodi hiyo baada ya kusemekana kutumia takribani dola za kimarekani milioni mia mbili kwa uandaaji wa kombe la dunia la mwaka 2022.

Uanzishwaji Wa Matumizi Ya Video Za Usaidizi Kwa Muamuzi (Var)

Kwa mara ya kwanza katika maisha ya kombe la dunia tangu kuanzishwa kwake kombe la dunia la mwaka 2018 ndio mashindano ya kwanza ya kombe la dunia ambayo VAR ilianza kutumia na kufanya maamuzi katika mechi mbalimbali. Mechi ya kwanza ambayo ilihusisha maamuzi ya VAR ni katika mchezo wa Ufaransa dhidi ya Australia baada ya muamuzi kutoa penalti kwa Ufaransa baada ya VAR kufanya maamuzi na mchezo kuisha kwa Ufaransa kushinda mabao mawili kwa moja.

Utolewaji Wa Tuzo Kwa Wachezaji

Katika kombe hilo la dunia mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane aliondoka na tuzo ya mfungaji bora kwa kuwa na jumla ya mabao sita huku, mchezaji bora akiwa ni Luka Modric kutokea Kroshia na mlinda mlango wa Ubelgiji Thibaut Courtois akiondoka na ‘Golden gloves’ kama mlinda mlango bora.

Kylian Mbappe Na Rekodi Yake

Kwa mara ya kwanza kushiriki katika kombe la dunia Kylian Mbappe mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa akaibuka na tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo baada ya kushiriki mashindano hayo akiwa na umri wa miaka 19. Mbappe amekuwa mchezaji wa pili duniani kushinda kipengele hicho akiwa na umri mdogo zaidi baada ya Pele aliyeshinda mwaka 1958 akiwa na miaka 18.

Ingizo Jipya La Washiriki Wa Kombe La Dunia

Wakati wa michuano hiyo ya kombe la dunia nchini Urusi, Iceland pamoja na Panama ndizo nchi mbili zilizoingia kushiriki kombe hilo la dunia kwa mara ya kwanza. Lakini kwa bahati isiyokuwa yao nchi zote mbili zilijikuta zikiishi katika hatua ya makundi baada ya kushika mkia katika makundi yao ambapo Iceland wao walikuwa kundi moja na nchi kama vile Argentina, Nigeria pamoja na Kroshia huku wao pamana wakishiriki kundi moja na nchi kama vile Ubelgiji, Uingereza pamoja na Tunisia.

Kuwepo Kwa Tuhuma Za Rushwa Pamoja Na Hongo

Baada ya Urusi kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa kombe hilo la dunia, nchi mabalimbali ikiwemo Uingereza zilitoa shutuma kwa Urusi na kusema ni nchi ambayo haijali haki za binadamu na pia hata nafasi yake ya uandaaji wa kombe hilo la dunia ni kutokana na kutoa hongo. Baada ya hayo mpelelezi kutokea nchi ya Marekani Michael J. Gracia akapewa kazi ya kuchunguza tuhuma hizo na baada ya kukamilika kwa ripoti hiyo ikawasilishwa na Jaji kutokea Ujerumani Hans Joachim Eckert, licha ya kuwepo kwa ripoti lakini bado pingamizi likaendelea wakati huo Shirikisho la soka duniani likiwa chini ya Sepp Blatter.

Leave your comment