Zifahamu Ngoma 5 Ambazo Diamond Platnumz Ameshirikiana Na Mbosso 

Mwandishi: Charles Maganga

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kama kuna ushirikiano wa kimuziki ambao mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva huufurahia basi ni pale ambapo CEO wa WCB Diamond Platnumz hushirikiana na Mbosso, msanii ambaye anajulikana sio tu kwa uwezo wake wa kuimba lakini pia kipaji chake kuandika. 

Ushirikiano huo mzuri unatokana na wawili hao kuwepo studio mara nyingi na kurekodi pamoja. Zifuatazo ni ngoma 5 kali ambazo Mbosso ameshirikiana na Diamond Platnumz : 

Oka 

Oka ni ngoma namba 9 kwenye EP ya Diamond Platnumz ya kuitwa First Of All na hii ni ngoma ambayo, kwa mara ya kwanza Mbosso alisikika akiimba muziki wa Lingala wenye asili ya huko nchini Congo. 

Video ya Oka imetayarishwa na Hanscana na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 11 kwenye mtandao wa YouTube 

Jibebe 

Kwenye ngoma hii Diamond Platnumz alipata jamala kutoka kwa Mbosso pamoja na Lavalava. Wimbo huu ulikuwa maarufu sana kutokana na ubunifu uliotumika kwenye mashahiri yake na pia ni wimbo ambao ulipendwa kwani kwa mara ya kwanza Mbosso alionekana akiimba wimbo wenye mahadhi ya Afrobeats. 

Yataniua 

Tangu kuachiwa kwake, ngoma ya Yataniua imepitia misukosuko mingi ikiwemo kuondolewa kwenye mtandao wa Youtube kutokana na sababu za hatimiliki yaani Copyrights. Kwa mara nyingine Mbosso alionesha uwezo wake wa kubadilika kwani kupitia ngoma hii alipita na upepo wa Amapiano, kitu ambacho pia alifanya kwenye ngoma ya Moyo.

Karibu 

Kutoka kwenye albamu ya Definition Of Love, Mbosso alimshirikisha Diamond Platnumz kwenye ngoma hii ambayo ndani yake Diamond na Mbosso wanasheherekea kuzaliwa kwa mtoto. Pamoja na kukosa video lakini hii ni ngoma ambayo ilifanya vizuri sana kwa mwaka 2021. 

Baikoko 

Video ya Baikoko iliweka rekodi mwaka 2021 baada ya kuwa video ya pili nchini Tanzania kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube baada ya Sukari ya kwake Zuchu. Ngoma hii imetayarishwa na Lizer Classic huku video ikiwa imeshughulikiwa na Director Kenny. 

Leave your comment