Ubashiri Mechi ya Chelsea Vs Manchester United

[Image Source: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

WIkiendi inaenda kuanza vizuri kwa mashabiki wa soka pale ambapo Chelsea wakiwa katika uwanja wa Stanford Bridge wanawakaribisha Manchester United Katika mzunguko wa 13 ligi kuu Uingereza Octoba 22.

Chelsea wakiwa nafasi ya nne wamepishana alama moja pekee na United wao wakiwa nafasi ya Tano na alama 23. Vigongo hawa wa darajani katika mechi tano za hapo awali kwa msimu huu ni mechi nne wameshisha na mechi moja wametoa sare sawa na mashetani wekundu ambao nao wameweza kushinda mechi nne na kutoa sare mechi moja.

Chelsea walishindwa kung’ara katika mechi yao dhidi ya Brentford baada ya kukubali sare ya bila kufungana na hii ni mechi ya kwanza kwa Graham Potter kutoa sare tangua ajiunge na Chelsea. Mpaka sasa majeruhi wa Chelsea ni pamoja na Wasley Fofana (goti), N’golo Kante (misuli ya paja),Reece James (kifundo cha mguu) pamoja na Conar Gallagher mwenye shida ya tumbo na unatarajiwa kuingia uwanjani muda wowote.

Ten hag bado anaendelea kumsugulisha benchi Cristiano Ronaldo baada ya kuwekwa benchi katika mechi ya United dhidi ya Tottenham Hotspurs na United kushinda bao mbili kwa sifuri. Katika kuelekea mchezo huu United hawana majeruhi mpaka sasa lakini nyota Cristiano Ronaldo ataukosa mchezo huo kutokana na utovu wa nidhamu katika mechi yao dhidi ya Spurs.

Wakiwa ndiyo mara kwa kwanza timu hizi mbili zinakutana kwa msimu huu wa ligi kuu Uingereza Chelsea na Manchester United katika mechi tano na ligi kuu Uingereza ni mechi nne wametoa sare na mechi moja United kaoondoka na ushindi hivyo basi odds za magoli kuwa zaidi ya moja ni 1.28

Leave your comment