Mfahamu Mshindi Wa Ballon D'or 2022 Karim Benzema

[Image Source: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Karim Mostafa Benzema ni mwanasoka katika timu ya Real Madrid ya Uhispania pamoja na  Timu ya Taifa ya Ufaransa katika nafasi ya mashambulizi. Benzema alizaliwa mnano mwaka 1987 huko Lyon Ufaransa na wazazi wenye asili ya Algeria ambapo baba yake aliitwa Hafid Benzema huku mama yake akiitwa Wahida Djebbara. Yafuatayo ni mambo saba pengine unaweza usiyafahamu kuhusiana na Benzema.

Imemchukua takribani miaka kumi na nne kuweza kushinda tuzo ya kwanza ya Ballon D’OR kama mchezaji bora ulimwenguni mwaka huu.

Tangu Benzema ajiunge na Real Madrid mnano mwaka 2009 ni usiku wa Octoba 17 2022 ndio siku ambayo Benzema ameweza kushinda tuzo ya kwanza ya Ballon D’or huku ndani ya miaka hiyo 14 Lionel Messi Pamoja na Cristiano Ronaldo wanajumla ya Ballon D’or kumi na mbili.

Karim hukamilisha moja kati ya nguzo tano za Uislam- Ramadhan

Mshambuliaji huyo akiwa ametokea katika familia ya Kiislamu na mara nyingi hushiriki Ramadhan kama moja ya nguzo za dini ya Kiislam. Katika kipindi hiki Benzema alisema hakumzui kufanya mazoezi yake na huwa anajisikia vizuri akiwa mfungoni.

Ana jumla ya vikombe 23 tangu ajiunge na REAL MADRID

Baada ya kujiunga na Real Madrid katika msimu wa mwaka 2009-2010 Karim Benzema amekusanya jumla ya mataji ishirini na tatu (23) akiwa na klabu hiyo ya soka. Katika vikombe hiyo  ubingwa wa Ulaya ameweza kuubeba mara tano, La Liga mara nne, Copa del Rey mara mbili, FIFA club world cup mara nne, UEFA Super Cup mara nne pamoja na Spanish super Cup ambapo ameweza kubeba ubingwa huo mara nne.

Rekodi ya kufunga goli la mapema katika mtanange wa EL Clasico

Desemba 2011 mshambuliaji huyo aliweza kufunga goli katika sekunde ya 22 ya mchezo katika badi ya EL Clasico ambayo inaihusisha timu ya Real Madrid pamoja na Barcelona na hakuna mwanasoka aliyeweza kuivunja rekodi hiyo mpaka sasa

Ushawishi wa kujiunga na timu ya Taifa ya Algeria

Wakati akiwa bado ni ua linalochanua Shirikisho la soka la nchini Algeria lilianza ushawishi wake kwa mshambuliaji huyo likitaka ajiunge na timu ya Taifa ya Algeria. Ijapokuwa wazazi wa Benzema ni watu wenye asili ya Algeria lakini Benzema aliamua kubaki Ufaransa na kukipika katika timu ya Taifa ya nchini humo.

Utolewaji wa Filamu inayoelezea maisha yake

Mnamo mwaka 2017 filamu iliyoelezea maisha ya Benzema ilitoka na kuonesha safari yake ya soka kuanzia Lyon mpaka alipofika Madrid. Filamu hiyo ilijulikama kama Le k Benzema iliyobeba uhalisia wa maisha ya soka pamoja watu wa karibu wakielezea maisha yake pamoja na undani kuhusiana na nyota huyo wa soka pia ukaribu wake na aliyekuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane Zizzou.

Uwepo wa ndugu ambao pia ni wanasoka

Akitokea katika familia ya watoto nane watatu wakiwa wakiume na watano wakiwa wanawake Karim pia ana wadogo wawili ambao pia wanajihusisha na kusakata kabumbu. Sabby pamoja na Gressy ni wadogo wa Benzema ambao pia wameamua kuchagua soka licha ya kuwa kiwango chao cha soka bado hakijaweza kumfikia kaka yao Maalim Karim Benzema.

Leave your comment