Ronaldo Afikisha Rekodi Ya Mabao 700

[Image Source: Manchester United/Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mshindi mara tano wa tuzo za Ballon D’or na mshambuliaji wa timu ya Manchester United Cristiano Ronaldo ameweza kujiwekea rekodi katika maisha yake ya soka baada ya kufanikiwa kufunga mabao mia saba ndani ya uwanja wa mpira akiwa na vilabu tofauti tofauti.

Ronaldo mwenye miaka thelathini na saba amefanikiwa kufunga mabao hayo akiwa na vilabu vinne tofauti vya soka ambavyo ni Sporting CP mabao matano, mabao mia moja kumi na nane akiwa na United kwa mara ya kwanza kabla ya kuhamia Real Madrid na kufunga mabao mia nne na hamsini, Juventus mabao mia moja na moja na sasa kwa mara nyingine tena akiwa na United ameweza kufunga mabao 26 tangu ajiunge na timu hiyo hapo msimu uliopita.

Pakua mixes Kali za Mziki wa Uganda ndani ya Mdundo

Katika maisha hayo ya soka na mabao hayo aliyoyafunga CR7 ameweza kunyakua vikombe mbalimbali katika ligi hizo nne pendwa zaidi duniani na hata katika mashindano ya kimataifa kama vile ubingwa wa Uingereza, ubingwa wa La liga, Ubingwa wa Serie A, Ubingwa wa Ulaya pamoja na vikombe vya ndani vya ligi hizo.

Ronaldo  akiwa na mabao hayo mia saba katika soka la vilabu bado hajatoa muda wake wa kuachana na soka na hii inaonesha ni kwa kiasi gani mwanasoka huyo mashuhuri bado anausongo na maisha ya kusakata kabumbu. Licha ya hayo yote Lionel Messi ambaye ni mshambuliaji wa timu ya PSG ya Ufaransa wiki iliyopita alitangaza baada ya kombe la dunia la Qatar ndilo litakuwa kombe lake la dunia la mwisho kushiriki. Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi ni wanasoka walioweka rekodi mbalimbali na wameonekana kushindanishwa sana kwa miongo miwili iliyopita.

Leave your comment