Ubashiri Mechi Ya Ureno Vs Uhispania

[Picha: telegraph.uc.uk]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Siku ya Jumanne Ureno Wanawakaribisha Uhispinia katika Uwanja wa manispaa wa jijini Braga. Mechi hiyo ni katika mzunguko wa 6 wa Ligi A ya mataifa Ulaya timu zote mbili zikiwa kundi la pili.

Katika kundi hilo la pili Ureno wanaongoza kwa kuwa na alama 10 wakifuatiwa na Uhispania ambao wao Wana jumla ya alama 08 wakifuatiwa na Uswizi wenye alama 06 huku Jamuhuri ya Czech ikishika mkia wakiwa na alama 04.

Katika michezo yao mitano ya Hapo nyuma timu hizi mbili walizokutana sare zilikuwa  4 na pia Uhispania walishinda mechi moja huku Ureno wakiwa hawana ushindi wa mechi yeyote Kati ya hizi tano.

Ureno wakiwa nyumbani katika mchezo huu baadhi ya wachezaji watakao wakosa ni pamoja na Joao Felix anayekipiga huko Atletico Madrid pamoja na Raphaël Guerreiro anayesumbuliwa na misuli ya paja.

Kwa upande wa wageni wa mchezo huo Uhispania wakiongozwa na mwalimu wao Luis Enrique wao hawana majeruhi wakati wakielekea katika mchezo huo.

Huu utakuwa moja Kati ya michezo yenye upinzani Sana kwa timu zote hivyo bas odds za magoli kuwa zaidi ya moja ni 1.35

Leave your comment