Graham Potter Kuinoa Chelsea

[Picha: Chelsea-news.co]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Graham Potter amesainiwa rasmi kuwa kocha katika kikosi Cha Chelsea. Hatua hii imekuja Mara baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel kutimuliwa mapema Jumatano ya wiki hii.

Kocha huyo raia wa Uingereza ameingia makubaliano na Chelsea akitokea Brighton and Hove Albion kwa mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Paundi milioni 50.

Siku ya Alhamisi mchana Potter akiwasili katika viunga vya mazoezi vya Chelsea na kusaini mkataba huo. Mkataba huo umekamilika baada ya Chelsea kukubaliana na Brighton kuwalipa kiasi cha Paundi milioni 16 ili kocha huyo aweza kujiunga na wababe hao wa London huko Stamford bridge.

Beki huyo wa Kati wa zamani mwenye Umri wa miaka 47 alianza safari yake huko Sweden katika timu ya Ostersund na kwenda Swansea City kabla ya mwaka mmoja baadaye kujiunga na Brighton.

Akiwa katika viunga hivyo vya Falmer stadium Potter ameisaidia Brighton kutokushuka daraja na pia kumaliza katika nafasi ya 9 kwa msimu uliopita huku katika msimu wa mwaka 2020-2021 walimaliza katika nafasi ya 16.

Sasa kibarua kimebaki kwa Brighton and Hove Albion kutafuta kocha mpya atakayeweza kukinoa kikosi hicho kwa msimu huu na kuendelea.

Leave your comment