Manchester United Wakamilisha Usajili Wa Winga Antony Dos Santos

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya purukushani za nenda rudi kuhusiana na usajili wa mchezaji Antony Matheus Dos Santos hatimaye sasa mchakato wa usajili wake umekamilika huko Old Trafford.

Mbrazili huyo aliyekuwa na nia ya kwenda United, taarifa ziliripoti kuhusu menejimenti ya Ajax kutotaka ajiunge na United na kufanya hata kupandishwa kwa dau la usajili wake.

Antony baada ya kuona Ajax wanambania akaamua kuonesha vipingamizi ikiwemo kususia mazoezi pamoja na baadhi ya mechi za timu hiyo ya huko Eredivisie side. Hakuishia hapo Antony aliomba mahojiano na Fabrizio Romano na kueleza hisia zake na jitihada za kutaka kuondoka Ajax licha ya kuwekewa vipingamizi.

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Meneja wa Ajax Alfred Schreuder alipozungumza na jarida moja alisema "sikuhizi kila kitu ni pesa, inasikitisha lakini hii ndiyo dunia yetu" alisema Schreuder. Kocha huyo hakuwa tayari kupoteza huduma ya winga hiyo.

Ajax imepokea Euro milioni 100 katika usajili huo. Hapo awali Euro milioni 90 zilikataliwa na Ajax wakati United walipohitaji kumsajili Winga huyo. Lakini mpaka sasa hatua za kimatibabu zimekamilika akiwa tayari amewasili Carrington Stadium.

United ijapokuwa wamekamilisha usajili huo lakini bado Cristiano Ronaldo inasemekana kunauwezekano wa kuondoka katika timu hiyo huku Frankie de Jong naye hakuna hatua zozote zenye matumaini ya usajili wake hivyo basi Antony anaweza kuwa bora zaidi katika matumaini ya safu ya mashambulizi ya kikosi cha Manchester United.

 

Leave your comment