Callum Hudson-odoi Ajiunga Na Bayern Leverkusen Kwa Mkopo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Hatimaye Bayern Leverkusen imetangaza rasmi kumsajili winga wa Chelsea Callum Hudson-odoi kwa mkopo kwa msimu huu mzima wa mwaka 2022/23.

Hii ni Mara ya kwanza kwa Odoi kucheza nje ya Chelsea tangu ajiunge na timu hiyo nwaka 2007 katika kituo Cha malezi ya watoto ( academy). Mnamo mwaka 2018 winga huyo ndipo alijiunga na timu ya kikosi kikuu Cha Chelsea.

Mchezaji huyo mwenye Umri wa miaka 21 inasemekana timu zaidi ya 20 barani Ulaya zilitamani kupata huduma yake lakini Leverkusen ndio waliokuwa bora kwake.

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kwa msimu uliopita Callum Hudson- Odoi alipata majeraha katika mechi waliyocheza na Luton Town katika mashindano ya FA na kumfanya akae nje ya mchezo wa soka kwa zaidi ya miezi kadhaa ili kutibu majeraha ya mgongo kutoka na udhaifu wa neva.

Akiwa Chelsea winga huyo tayari amecheza mechi 126 na kupata mabao 16 pia kutengeneza pasi 22 za usaidizi wa magoli katika klabu hiyo.

Ushiriki wa Callum Hudson-odoi umeisaidia Chelsea kushinda mashindano mbalimbali Kama vile Ubingwa wa Ulaya, ubingwa wa FA, ubingwa wa klabu Bora ya dunia, na pia ubingwa wa Europa.

Leave your comment