Nyimbo Mpya: Zuchu 'Fire', Kizz Daniel 'Buga' na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mtandao wa Youtube umeendelea kuwa kipimo kikubwa cha kazi za wasanii kwa hapa nchini Tanzania ambapo kwa wiki hii ngoma mbalimbali zimeendelea kushika nafasi ya juu katika mtandao huo maarufu baada ya mashabiki kuweza kuzisikiliza zaidi.

Zifuatazo ni ngoma tano ambazo zinafanya vizuri katika mtandao wa YouTube kwa wiki hii:

Fire - Zuchu.

Ngoma ya "Fire" ya kwake Zuchu imeweza kuwasha moto huko Youtube kwa wiki hii. Ngoma hii inapatikana kwenye project ya Zuchu ya kuitwa 4.4.2 na pamoja na kukosa video lakini kufikia sasa imshatazamwa na kusikilizwa mara Milioni 1.4 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=lpBr-zmQG4g

Te Quiero - Rayvanny Ft Marioo

Zimetimia siku takriban 14 tangu Rayvanny aachie video ya  Te Quiero na tangu kuachiwa kwake, video hii ambayo imegharimu Milioni 100 za kitanzania imeonekana kupendwa sana na mashabiki kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.2 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=w8MsgMIL3qE

Buga - Kizz Daniel Ft Tekno

Ukiweka kando mitindo ya kuvutia dansi katika video ya Buga ya kwake Kizz Daniel, kitu kingine kilichovutia ni namna ambavyo Director TG Omori ameweza kuhusisha tamaduni na bendera za nchi mbalimbali za Afrika katika video hii ambayo ndani ya wiki mbili tu tayari imeshakusanya watazamaji Milioni 18 huko Youtube

https://www.youtube.com/watch?v=bLF90M96m2Q

Ukizaliwa - Stamina Ft Banana Zorro

Ngoma hii ni episode ya pili kutoka kwenye project ya Stamina ya kuitwa "Love Bite". Itoshe kusema video ya ngoma hii ambayo inamuonesha Stamina akiwa anampa nasaha mwanaye ambaye bado hajazaliwa, imeweza kufanya vizuri kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara laki tatu thelathini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=6VHBO5l4It4

Jaro - Zuchu

Kwa mara nyingine tena, Zuchu ameendelea kutikisa Youtube na Jaro, ngoma ambayo ndani yake anasifu namna ambavyo mpenzi wake anampenda na kumthamini kiasi cha kuvutiwa na vitu ambavyo Zuchu anaona ni udhaifu. Hii ni ngoma ambayo inapatikana kwenye 4.4.2 na kufikia sasa imeshatazamwa mara laki nne na elfu sita huko Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=abaJcRUGz7A

Leave your comment