Ubashiri Mechi Ya Liverpool Vs Manchester United- Bangkok

[Picha: thesportsgrail.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Balaa lingine la mechi za kabla ya msimu zinaanza tena. Jumanne hii Majogoo wa London wanavaa Tena na mashetani wekundu huko Bangkok katika mechi za kabla ya msimu.

Liverpool wao wakiwa na kocha wao yule yule Jürgen Klopp huku wao Manchester United rasmi wakiwa wamemkaribisha Erik Ten Hag wanavaana katika uwanja wa Rajamangala.

Liverpool katika ziara hiyo Hakuna mchezaji aliyetia udhuru ya namna yoyote ile. hivyo wachezaji wote waliopangwa kuwepo katika ziara hiyo tayari wamewasili huko Bangkok.

Ila kwa upande wa Mashetani wekundu wao bado benchi lao la wachezaji  limeendelea kupata Moto. Hii imetokana na kuwa mchezaji wao Cristiano Ronaldo kutokusafiri na kikosi hicho Cha wachezaji wenza.

Sababu iliyotolewa ni kuwa na matatizo ya kifamilia. Ila kwa tetesi za mitandaoni zinazovuma kwa Kasi ni kuwa mshambuliaji huyo anahitaji kuondoka huko Old Trafford.

Liverpool katika majira haya ya usajili ya dirisha kubwa la majira ya joto Hakuna changamoto waliyoipitia katika sajili zao.

Ila Kwa upande wa United wao sajili zao zimeleta kusuasua na hii ni kutokana na wachezaji Kama Frenkie de Jong kutotaka kujiunga na timu hiyo.

Ten Hag bado ana kibarua Cha kuimarisha timu hiyo ambayo mpaka Sasa hata mashabiki hawana Imani nayo.

Katika ziara hiyo ya kueleka huko Bangkok Liverpool wamesafiri na kikosi Cha takribani watu 37 huku wao United wakisafiri na kikosi Cha watu 31.

Katika mechi hiyo Liverpool Huenda wakawakaribisha uwanjani wachezaji wao wapya waliowasajili katika majira haya ya joto ambao ni Darwin Nunez, Fabio Carvalho pamoja na Calvin Ramsey.

Na kwa upande wa Manchester United ijapokuwa Kuna migongano ya usajili bado lakini tayari wamesha msajili mchezaji kutokea Feyenoord Tyrell Malacia. Huku Harry Maguire akiendelea kuwa kiongozi wa kikosi hicho.

Katika mechi hii ambayo timu zote mbili zinakipiga zikiwa katika ardhi ya ugenini Odds za magoli kuwa zaidi ya moja ni 2.85

Leave your comment