Nyimbo Mpya: Ibraah 'King of New School album', '4.4.2' Zuchu na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mambo yamezidi kuwa sukari sana kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva wiki hii na hii ni baada ya wasanii wakubwa kwa wadogo kuachia bidhaa mpya sokoni ambazo zineweza kukonga hisia za mashabiki na kuzidi kuchangamsha "gemu" la Bongo Fleva.

Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka wasanii wa Tanzania wiki hii.

Te Quiero (Video) - Rayvanny Ft Marioo

Rais wa Next Level alishangaza mashabiki zake wiki baada ya kuachia video ya Te Quiero. Kwa mujibu wa Rayvanny alisema kuwa video imegharimu takriban Milioni 100 mpaka kukamilika kwake. Video hii imeundwa na stori nzuri ambayo inamuonesha Rayvanny na abiria wenzake wakiwa wametekwa kwenye ndege na baada ya kupelekwa sehemu isiyojulikana, Rayvanny anaonekana kuzama kwenye penzi na mwanadada aliyekuwemo kati ya abiria hao hivyo kutoroka nae.

https://www.youtube.com/watch?v=w8MsgMIL3qE

The King Of New School (Album) - Ibraah

Baada ya kuitangaza kwa muda mrefu, hivi karibuni bila taarifa Ibraah alitetemesha Bongo Fleva na ngoma yake ya The King Of New School. Hii ni albamu ya kwanza ya Ibraah tangu aanze muziki na ameweza kushirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo AV na Bracket kutokea Nigeria, Maudi Elka kutokea DRC Congo pamoja na Christian Bella kutokea hapa nchini Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=RsQyHXRm7DQ

Ukizaliwa - Stamina Ft Banana Zorro

Wiki hii Stamina aliachia ngoma ya "Ukizaliwa" ambayo ni sehemu ya pili ya series yake ya kuitwa "Love Bite". Kwenye ngoma hii Stamina anavaa uhusika wa mwanaume ambaye anapata mtoto akiwa bado hajajipanga na kipindi mkewe akiwa anatarajia kujifungua Stamina anachukua muda wake kumpa mawaidha mtoto wake kuhusu maisha kabla hajazaliwa.

https://www.youtube.com/watch?v=6VHBO5l4It4

4.4.2 - Zuchu

Kunako WCB, bingwa wa kuandika ngoma za mapenzi, Zuchu hatimaye ameachia ngoma zake mbili ambazo ni "Jaro" na"Fire" ambazo zinapatikan kwenye project yake ya kuitwa 4.4.2. Kwenye Jaro Zuchu ametumia Kiswahili na Kiingereza kufikisha ujumbe wake ilhali Fire ni ngoma, ambayo Zuchu ametukumbusha uwezo wake wa kuandika na kuimba ngoma zenye asili ya Baibuda.

https://www.youtube.com/watch?v=lpBr-zmQG4g

Star Remix - Mabantu Ft Rayvanny

Baada ya Utamu Remix ambayo walimshirikisha Harmonize kufanya vizuri hatimaye Mabantu wamerudi tena Star Remix akiwa na Rayvanny. Mdundo, midondoko na ujumbe wa ngoma hii hasa kwenye kipande cha Rayvanny ambao baadhi wameutafsiri kama salamu za Rayvanny kwa Harmonize zimependezesha sana ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=IZub_PrZZ4w

Leave your comment