Nyimbo Mpya:Zuchu Aachia Nyimbo Mbili Mtawalia 'Fire' na 'Jaro'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Zuchu hivi karibuni amekata kiu ya mashabiki zake baada ya kuachia ngoma mbili ambazo ni Jaro pamoja na Fire, ngoma ambazo zinapatikana kwenye project yake ya kuitwa 4.4.2.

Zuchu ambaye anajulikana kwa uandishi wak mzuri ameachia ngoma hizo hivi karibuni ikiwa ni takriban miezi mitano tangu aachie ngoma yake ya mwisho ya kuitwa "Mwambieni".

Ikumbukwe kuwa wiki moja iliyopita Zuchu alitangaza kuachia ngoma mbili ambazo ni Jaro na Fire ambazo Zuchu aliweza kuziweka kwenye project moja aliyoiita 4. 4.2 ikiwa ni mara ya pili kwa msanii huyo kuachia ngoma mbili kwa mpigo kwani Mwezi Septemba mwaka 2020 Zuchu aliachia ngoma mbili ambazo ni "Cheche" na "Litawachoma" ambazo aliziweka kwenye project moja ya kuitwa "Side 2 Side".

Ngoma ya kwanza kwenye project ya 4.4. 2 inaitwa "Jaro". Hii ni ngoma nzuri ya mapenzi ambayo ndani yake Zuchu anajivunia na kutamba kuhusu mapenzi motomoto anayopewa na mwandani wake. Wimbo huu ulikuwa ni maarufu kabla haujaingia sokoni kwani Zuchu aliutumbuiza kwenye tamasha la Africa Dag Benefit Concert huko Lagos Nigeria mwezi mmoja uliopita. Ngoma hii imetayarishwa na Mocco Genius.

Kwa upande wa "Fire" hii ni ngoma kali ya Bongo Fleva ambayo Zuchu pia anaonesha alivyozama kwenye penzi zito. Ngoma hii ambayo imepambwa ni Kiswahili cha kipwani imetayarishwa na Trone, mtayarishaji wa muziki ambaye pia ametayarishwa ngoma ya "Sukari" ya kwake Zuchu.

Baada ya project hii ya 4.4.2 baadae mwaka huu, Zuchu anatarajiwa kuachia albamu yake ya kwanza ambayo kufikia sasa bado hajafichua jina lake wala tarehe ya kuiachia.

https://www.youtube.com/watch?v=lpBr-zmQG4g

Leave your comment