Nyimbo Mpya: Hatimaye Rayvanny aachia Video ya Wimbo "Te Quiero" aliomshirikisha Marioo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki nguli kunako ulingo wa Bongo Fleva Rayvanny hatimaye ametuliza kiu ya mashabiki zake ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiiulizia video ya Te Quiero, ngoma ambayo amemshirikisha mtoto wa Mama Amina yaani Marioo.

Kama ambavyo Rayvanny alisema kuwa video yake inayofuata baada ya "I Miss You" itakuwa ni ya kihistoria basi bila shaka hakukosea. Video ya Te Quiero imeundwa na stori ya kusisimua ambapo Rayvanny akiwa na abiria wenzake wanaonekana wakiwa wametekwa kwenye ndege waliyopanda na kisha kupelekwa kusikojulikana na watekaji hao na katika sakata lote hilo, Rayvanny anaonekana kuzama kwenye penzi zito na mwanadada mmoja.

Utunzi wa mzima wa stori ya Te Quiero, uhalisia wa wahusika na mandhari yaliyotumika lakini kikubwa zaidi ubora wa picha umefanya video hii kuwa bora sana na kwa mujibu wa Rayvanny ametanabaisha kuwa video hii imegharimu takriban Milioni 100 mpaka kukamilika.

Video ya Te Quiero imeongozwa na Director Eris Mzava ambaye anajulikana kwa kufanya kazi lukuki na Rayvanny ikiwemo Jennifer Remix ambayo Rayvanny alimshirikisha Guchi pamoja na Te Amo ngoma ambayo iliingia sokoni takriban miaka miwili iliyopita.

Te Quiero ni muendelezo wa Rayvanny kuendelea kuachia video kali kwani takriban mwezi mmoja uliopita msanii huyo aliachia "I Miss You" video ambayo imegharimu takriban Milioni 100.

https://www.youtube.com/watch?v=w8MsgMIL3qE

Leave your comment