Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Ngoma Mpya "Dear Ex"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania Marioo kwa mara nyingine tena amepamba kiwanda cha muziki nchini Tanzania baada ya kuachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa "Dear Ex"

Marioo ambaye pia anajulikana kama mfalme wa Amapiano ameachia "DearEx" ikiwa ni miezi miwili tangu mwanamuziki huyo kuachia ngoma yake ya "Naogopa" ambayo amemshirikisha CEO wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize.

Kwenye "Dear Ex" kwa mara nyingine tena Marioo anarukia kwenye muziki wa Amapiano ambapo katika ngoma hii ambayo imetayarishwa na Tony Duardo Marioo anatanabaisha namna ambavyo anasumbuliwa na mpenzi wake wa zamani na anatumia maneno ya kuudhi kuonesha kuwa hahitaji tena mahusiano na ex wake.

Bado Marioo hajaachia video ya ngoma hii lakini kufikia sasa mashabiki wengi wameonekana kuipokea vizuri ngoma hii ambayo ni ya pili kwa Marioo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2022.

Aidha Dear Ex ni Amapiano ya tatu kutoka kwa Marioo baada ya 2020 kuachia Mama Amina aliyomshirikisha Sho Madjozi na Bontle Smith huku 2021 mwanamuziki huyo aliachia "Bia Tamu" ngoma ambayo ilifanya vizuri sana kiasi cha kushinda tuzo ya Ngoma Bora Ya Bongo Fleva kwa  kwenye Tanzania Music Awards kwa mwaka 2022.

Kando na Marioo wasanii wengine ambao pia wameshafanya ngoma za Amapiano ni pamoja na Rayvanny, Diamond Platnumz, Baba Levo, Damian Soul, Zuchu pamoja na Mbosso ambaye siku chache zilizopita aliachia "Moyo"  Amapiano ambayo amemshirikisha Costa Titch na Phantom Steeze kutokea Afrika.

https://www.youtube.com/watch?v=vmv_0Fpw5zk

Leave your comment