Orodha Ya Wachezaji Wanaotikisa Usajili Ligi Ulaya
27 June 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Ikiwa bado dirisha la majira ya joto likiwa linaendelea kusukuma gurudumu, Timu nyingi zinaendelea kukimbizana ili kuwapata wachezaji wanaotakiwa kutengeneza vikosi vitakavyo kuwa Bora zaidi katika misimu wa 2022/23. Wafuatao ni wachezaji wanaotakiwa kuagana na timu zao kwa msimu huu na kujiunga na timu zingine.
Robert Lewandowski
Kinara wa magoli Bundesliga, Robert Lewandowski (33), anatarajiwa kukimbilia La liga na kwenda kukichapa huko Barcelona ikiwa bado Barcelona hawajapata saini yake lakini tayari straika huyo kutokea Poland ameonesha Nia yake ya dhabiti kabisa kuondoka katika Klabu hiyo ya Bayern Munich ambao hawako tayari kumuacha ajiunge na timu nyingine. Lewandowski kwa Sasa ndio chaguo la kwanza kwa Barcelona huku Bayern wakiwa wanahitaji kiasi cha Pound milioni 43 ili waweze kuagana na straika huyo. katika mechi 46 alizozicheza akiwa na Bayern kwa msimu uliopita Lewandowski ameweka kambani jumla ya magoli 50 na kumfanya awe kinara wa magoli Bundesliga.
Soma pia: "Akothee The Lioness" Album Review
Sadio Mane
Baada ya kujiunga na Liverpool 2016 Sasa winga huyo kutokea Senegal, Sadio Mane anatarajiwa kuagana na timu hiyo katika majira haya ya kiangazi na kujiunga na Bayern Munich ya Ujerumani. Mane ambaye tayari ameshapata mataji na Vikombe takribani vyote akiwa na Liverpool Sasa anajiunga na vinara hao wa Bundesliga kwa dau la Paundi milioni 35. Kwa mujibu wa Mane kuondoka kwake Liverpool ni ili akatafute changamoto zingine na pia Mane anaenda kuliziba pengo wa Lewandowski anayetarajiwa kuhamia Barcelona.
Gabriel Jesus
Arsenal wako mbioni kuisaka saini na mshambulia wa Manchester City, Gabriel Jesus ambaye pia anaonesha Nia ya kutaka kuondoka klabuni hapo. Wawakilishi wa Jesus wanatarajiwa kukaa mezani na kujadili suala la Jesus kwenda kukipiga Arsenal kwa msimu ujao. Huku kocha wa Arsenal Mikel Arteta akionesha umuhimu wa kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya kuondoka kwa washambuliaji wawili katika kikosi hicho Cha Arsenal ambao ni Pierre-Emerick aubameyang pamoja na Lacazette.
Romelu Lukaku
Baada ya kusajiliwa na Chelsea mapema mwezi wa 8 mwaka Jana Mshambuliaji wa timu hiyo ya Chelsea Lukaku anatarajiwa kurejea Tena Inter Milan kwa mkopo, hii ni baada ya kutokuwa na msimu mzuri akiwa Chelsea na Tuchel kutokuwa na matumizi nae kwa msimu huu licha ya Chelsea kutokufanya usajili wowote mpaka Sasa. Kiasi cha l
Poundi milioni 9 kinaweza kumfanya Lukaku arejee Tena Inter Milan kwa mkopo.
Leave your comment