Uchambuzi Mechi Ya Yanga vs Coastal Union

[Picha: goal.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kabla ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania NBC Premier League kuisha tayari timu ya 'Wananchi' Young African Sports club wameshatangazwa kuwa mabingwa wa Ligi hiyo baada ya ushindi wa mechi yao dhidi ya Coastal Union ya Tanga kwa ushindi wa bao 3-0 mechi iliyochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika msimu huu wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga wamecheza mechi 25 Kati ya zile 30 na mpaka Sasa Hakuna mechi yoyote ile waliyofungwa na hii ikapelekea wao waweze kushinda ubingwa huu katika dakika za mapema kabisa.

Soma pia: Sababu Za Haaland Kujiunga Na Manchester City

Ubingwa huo wa Yanga umekuwa ni ubingwa wao wa 28 na kuwa wao ndio vinara wa Ligi kuu Tanzania bara, kwani Yanga katika mechi hizo 25 mpaka Sasa ni mechi 20 walizoshinda na mechi 7 ndizo walizotoa sare.

Katika mechi yao dhidi ya Coastal Union katika pindi Cha kwanza tu Cha mchezo Yanga walimiliki mpira kwa 56% huku Coastal wao wakimiliki mpira kwa 44%, kwa upande wa mashuti ya moja kwa moja Yanga walikua na Mashuti 4 ya moja kwa moja kuelekea lango la Coastal huku wao Coastal wakiwa hawana shuti lolote la moja kwa moja katika lango la Yanga.

Katika mechi hiyo ilionesha kujaa na utulivu kwani katika dakika zote 90 Hakuna kadi yoyote iliyotolewa katika pande zote mbili za timu hizo, huku suala ya kona timu zote 2 yaani Yanga pamoja na Coastal Union walikuwa na Kona 7 kwa pande zote 2.

Leave your comment