Orodha Ya Wachezaji 5 Waliosajiliwa Kwa Gharama Zaidi EPL

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Ikiwa bado wimbi la usajili likiendelea kutimua vumbi huko Uingereza, Rekodi mbalimbali zimeendelea kuwekwa na wachezaji wa soka katika Ligi ya EPL baada ya mamilioni ya Fedha kutolewa ili timu ziweze kufanya usajili kama moja ya hatua za kuboresha timu zao ili ziweze kufanya vizuri zaidi.

Wafuatao ni wanasoka walioweza kuweka rekodi za usajili kwa kusajiliwa kwa gharama zaidi katika Ligi kuu ya Uingereza EPL.

1. Jack Grealish

Baada ya Agosti mwaka 2021 Manchester City kutangaza kuopoa saini ya Jack Grealish, Aston Villa walipokea dau la Paundi milioni 100 kwa mkataba wa miaka 6 na kumfanya kiungo mshambuliaji pamoja na winga huyo kuwa mchezaji wa kwanza kutokea EPL aliyesajiliwa kwa dau refu zaidi.

Baada ya usajili huo Grealish alipewa jeshi namba 10 ya moja kati ya mashujaa wa Manchester City Sergio Aguero na ndiyo namba anayoitumia hadi Sasa akiendelea kukipiga katika viunga vya Etihad Stadium.

2. Romelu Lukaku

Anaweza kuonekana Kama mchezaji aliyefanyiwa usajili mkubwa na wa ghali zaidi katika Ligi ya Uingereza kutokana na kuingia katika orodha hii Mara mbili tofauti, Lukaku baada ya kufanyiwa usajili mkubwa akiwa na Manchester United akitokea Everton, lakini pia alisajiliwa katika dirisha kubwa na Chelsea akaitokea Inter Milan kwa kiasi cha paundi milioni 97.5 katika msimu wa mwaka 2021/22 na mpaka Sasa bado Yuko na klabu hiyo kutokea Stanford bridge ijapo kuwa kuna tetesi za yeye kutaka kurejea tena Serie A.

3.Paul Pogba

Baada ya kuondoka Manchester United akiwa Kama mchezaji huru katika msimu wa mwaka 2012/13 na kuelekea Juventus ,Paul Pogba alirejea Tena United akitokea Juventus ya Italia na ndipo United walipotoa kiasi cha Paund milioni 93.25 na kumfanya awe mchezaji wa pili aliyesainiwa na United kwa dau kubwa zaidi licha ya kuwa katika msimu huu Pogba anaondoka Tena United Kama mchezaji huru baada ya kukataa kuongeza mkataba na Mashetani hao Wekundu.

4. Darwin Nunez

Akiwa bado ni kinda wa miaka 22, Nunez Sasa amekimbilia viunga vya Liverpool na kujiunga na Majogoo wa London baada ya kudumu Benfica kwa takribani miaka miwili.

Liverpool wametoa takribani dau la Pound milioni 85 kwa Benfica ili mshambuliaji huyo aweze kujiunga na Liverpool kwa msimu ujao wa mwaka 2022/23, na kiasi hicho kinamfanya awe mchezaji wa tano aliyesajiliwa kwa dau kubwa zaidi EPL.Usajili huu wa Nunez ni wa kwanza kwa msimu huu Kama mshambuliaji na hii inaonesha ni kwa jinsi gani Klopp anahitaji ushindi zaidi kwa msimu inaikaribia kuanza.

5. Harry Maguire

Akiwa bado ni nahodha wa timu ya Manchester United, licha ya kuwa na msimu usio mzuri kwake kutokana na vitusho kutoka kwa mashabiki, Harry Maguire ni moja kati ya wachezaji ambao waliifanya United kutoa kiasi kikubwa Cha fedha baada ya Ole gunnar solskjaer  kuona ndiye mchezaji atakayeweza kuisaidia United katika safu yake ya ulinzi.

Takribani kiasi cha Pound Milioni 80 United walizimwaga kwa Leicester City ili waweze kumpata Maguire mwaka 2019.

 

 

 

 

Leave your comment