Ifahamu Klabu ya Simba SC Ya Nchini Tanzania

[Picha: Simba SC Facebook]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya kusitisha mkataba wake na kumtimua aliyekuwa na kocha wao Pablo Martin Sasa klabu ya Soka ya nchini Tanzania Simba Sc imeanza kuingia sokoni na kusaka wachezaji watakao husika na kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2022/23, Mkakati huu ulipangwa na kocha huyo pamoja na menejimenti ya timu hiyo na mmoja wa wachezaji hao ni mshambuliaji ambaye atatoka nje ya nchi na Sasa ni Mzambia Mmali Allasane Diarra, na Hilo linaweza kutokana kuonekana kwa dalili za klabu hiyo kuonesha kunyang'anywa ubingwa kwa msimu huu na mahasimu wa Young African Sports club.

Soma pia: Washindi Tuzo za PFA 2021/22

Kuanzishwa kwa  klabu ya Simba SC

Simba sports Club ni timu ya mpira wa miguu iliyoanzishwa mwaka 1936 ambayo iligawanyika kutoka kwa Young African Sports club kwa Sasa wakiwa watani wa jadi. Simba sports Clubs alimaarufu Kama Wekundu wa msimbazi wakati wa kuanzishwa kwake ilijulikana Kama Eagles na baadaye wakabadili jina na kujiita Sunderland na ilipojiri mwaka 1971 ndipo wakaamua kubadili jina na kujiita Simba Sports club na "NGUVU MOJA" ndiyo kauli mbiu yao.

Uwanja wa Benjamin Mkapa ndio uwanja wake wa nyumbani ijapokuwa uwanja huo ni Mali ya serikali lakini Simba huutumia uwanja huo kutokana na Hali ya kuwa mpaka Sasa Simba hawana uwanja wake wanaoumiliki, Makao  makuu kabisa ya timu hiyo  ni Kariakoo huko Msimbazi yakiwa ndio maeneo yao ya kujidai.

Kuanza kushiriki ligi mbalimbali

Ikiwa bado chini ya jina la Sunderland, mwaka 1965 wakati Ligi kuu inaanzishwa, Simba ilichukua kombe la kwanza la Ligi kuu kwa wakati huo ikiwa inaitwa National League kabla ya kuitwa Tanzania Premier League mwaka 1997 Simba ikiwa bado ni mshiriki wa Ligi hiyo kwa misimu yote bila ya kushuka daraja kwa kipindi chote hicho, Simba pia imeshashiriki ligi ya klabu bingwa Afrika, CECAFA na mashindano ya CAf katika Ligi za nje.

Umiliki wa klabu hiyo

Umiliki wa klabu hiyo kongwe barani Afrika umegawanyika katika pande mbili kwa Sasa kwani 51% ya klabu hiyo iko chini ya wajumbe  wanaowakilisha wanachama wao katika klabu hiyo huku 49% ya umiliki wa klabu hiyo iko chini ya Mohammed Dewji aliyewekeza katika klabu hiyo takribani shilingi za kitanzania Billion 20 Kama sehemu ya hisa zake katika klabu hiyo ijapo kuwa alitakiwa atoe kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 19.6 Ila ongezeko la bilioni 0.4 ni kutokana na mapenzi yake juu ya klabu hiyo ya Simba kwa mujibu wake Dewji.

Mafanikio katika ya klabu ya Simba

Simba ikiwa ni moja kati ya klabu Bora barani Afrika imepata mafanikio mengi Sana katika kipindi Cha miaka 84 tangu kuundwa kwake. Mpaka Sasa tayari klabu hiyo imeweza kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Mara 22, Vikombe 5 vya kombe la FA, wamekuwa washindinwa ngao ya Jamii Mara 9,  na pia Simba wameshawahi kushinda michuano ya CECAFA na kushinda Mara 6 huku pia wakiwa wameshawahi kushiriki mashindano makubwa ya klabu bingwa Afrika na pia kombe la Shirikisho na kwa msimu huu wa 2021/22 katika kombe hilo la Shirikisho wameishia katika hatua ya robo fainali.

Ubora wa klabu ya Simba

Simba imekuwa moja ya vilabu Bora Tanzania pamoja na barani Afrika mpaka sasa, Kwa Afrika Simba inashikilia nafasi ya 11 Kama moja ya vilabu Bora barani Afrika huku duniani ikiwa inashikilia nafasi ya 130 na hii ni kwa mujibu wa Shirikisho pa kimataifa la historia ya mpira wa miguu pamoja na takwimu (IFFHS).

Uthamani wa klabu ya simba

Mpaka Sasa Hakuna takwimu za halali za kudhihirisha udhanami wa klabu hiyo lakini kwa makadirio yasiyo rasmi tangia mwekezaji Mohammed Dewji apewe kibali Cha kuwa na hisa katika klabu hiyo inasemekana kukadiria kiasi cha shilingi bilioni 40 za kitanzania.

 

Leave your comment