Washindi Tuzo za PFA 2021/22
13 June 2022
[Picha: skysports.com]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
June 9 ilikuwa siku maalum kwa tuzo za Professional Football Awards kutolewa katika msimu huu wa 2021/22 na mwishoni mwa mwezi wa tano Mohamed Salah, mchezaji wa Liverpool alishuhudiwa akibeba tuzo mojawapo katika kipengele Cha PFA Fans Award akiwa ndiye mchezaji aliyeonesha kuwa chaguo pendwa zaidi kwa mashabiki wa soka katika Ligi kuu ya Uingereza.
Wafuatao ni washindi waliopata tuzo hizo za PFA Awards kwa msimu huu pamoja na vipengele walivyoshiriki.
Tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka
Akiwa ni moja kati ya wachezaji Saba walilopata tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo, Mohamed Salah katika msimu wa mwaka huu 2021/22 ameweza kubeba tena tuzo ya PFA Player of The Year Award baada ya msimu uliopita kuondoka Tena na tuzo hiyo kutokana na mchango katika Ligi kuu ya Uingereza.
Sala katika msimu huu amekua mfungaji Bora akiwa sawa na mchezaji wa Tottenham Son Heung Min kwa kufunga jumla ya mabao 23 na akiwa ametengeneza jumla ya pasi za usaidizi wa magoli 13.
Katika kipengele hicho Sala alikuwa akichuana na Kelvin de Bruyne wa Manchester City, Cristiano Ronaldo wa Manchester United, Harry Kane kutokea Tottenham Hotspurs pamoja na Virgil Van Dijk na Sadio Mane kutokea Liverpool.
Download FREE DJ Mixes on Mdundo
Tuzo ya mchezaji bora wa kiume mwenye umri mdogo
Tuzo hii ikiwa imeenda kwa kinda wa Manchester City Phil Foden mwenye umri wa miaka 22. Foden ameichukua tuzo hii akiwa mchezaji wa 5 kubeba tuzo hii Mara 2 mfululizo baada ya msimu uliopita kuondoka Tena na tuzo hiyo. Kinda huyo wa Pep Guardiola katika msimu huu ameweza kufunga jumla ya mabao 9 na kutoa pasi 5 za usaidizi wa magoli.
Katika kinyang'anyiro hicho Foden alikuwa akichuana na Reece James wa Chelsea, Jacob Ramsey tokea Aston Villa, Conor Gallagher wa Cristal Palace huku Bukayo Saka pamoja na Emile Smith Rowe wao wakiwa wanakipiga katika Klabu ya Arsenal.
Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka
Mchezaji wa timu ya wanawake ya Chelsea, Sam Kerr ndiye nchezaji aliyeshinda tuzo hiyo kwa msimu huu, Kerr kwa msimu huu ameweza kuweka kambani jumla ya mabao 20 na pia ameisaidia timu take ya Chelsea kushinda ubingwa wa FA baada ya kuifunga timu ya wanawake ya Manchester City.
Katika kipengele hicho waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni Lauren Hemp pamoja na Alex Greenwood wa Manchester City, Pernille wa Chelsea, Vivianne Miedema na Kim Little Hawa wakitokea Arsenal.
Tuzo ya mchezaji bora wa kike mwenye umri mdogo
Manchester City imeonekana kuwa na wachezaji bora wenye umri mdogo kwa msimu kwani hata tuzo hii imeenda kwa mwanadada Lauren Hemp mwenye umri wa miaka 21 na hii ikiwa siyo Mara yake ya kwanza kushinda tuzo hiyo lakini hii imekuwa Mara yake ya 4 kubeba tuzo hiyo.
Katika msimu huu mshambuliaji huyo amefunga jumla ya magoli 16 akiwa na Manchester City.
Katika kinyang'anyiro hicho Hemp alikuwa na wachezaji wengine Kama Ella Toone wa Manchester United, Frida Maamum kutokea Arsenal, Lauren James wa Chelsea pamoja na Maya Le Tissier kutokea Brighton.
Kikosi bora cha mwaka(wanaume)
Katika kikosi cha mwaka kilichopangwa na PFA kwa upande wa wanaume zaidi ya nusu ya kikosi hicho wachezaji wake wanatokea katika timu ya Liverpool na wachezaji hao ni Mohamed Salah, Sadio Mane, Thiego Alcantara, Trent Alexander Arnold, Virgil Van Dijk, pamoja na mlinda mlango wao Alisson Becker, huku wachezaji watatu ni kutoka Manchester City ambao ni Bernardo Silva, Kelvin de Bruyne, Joan Cancelo wengine ni Cristiano Ronaldo wa Manchester United, pamoja na Antonio Rudriger beki wa Kati wa Chelsea.
Kikosi bora cha mwaka kwa upande wa wanawake
Katika kikosi Bora Cha wanawake mshindi wa kiatu Cha dhahabu Sam Kerr ameongoza kikosi hicho pamoja na wachezaji wenza wa timu ya Chelsea ambao ni Ann-katrin Berger, Millie Bright na Guro Reiten, huku wachezaji wengine ni kutoka Arsenal ambao ni Kim Little, Lea Williamson, pamoja na Vivianne Miedema, huku Manchester City wao wakiwa na wachezaji watatu katika kikosi hicho ambao ni Alex Greenwood, Caroline Weir pamoja na mshindi wa tuzo ya mchezaji mwenye umri mdogo kwa upande wa wanawake Lauren Hemp pia Manchester United hawakua nyuma Sana kwani wao katika kikosi hicho mchezaji wao Ona Batlle naye Yuko kikosini.
Tuzo ya heshima ( wanaume)
Katika kipengele hiki Cha PFA Merit Awards tuzo hii umegawanyika katika makundi mawili kwani katika tuzo hii kuna tuzo ya HESHIMA upande wa wanaume pamoja na tuzo ya heshima kwa upande wa wanawake.
Kwa upande wa wanaume tuzo hii imeenda kwa Roy hodgson ambaye amekuwa kocha katika timu 22 nchi 8 tofauti lakini tuzo hii ameibeba juu ya mchango wake katika timu ya Watford amabayo ndio timu alipostaafu Kama kocha katika Soka mapema mwaka huu.
Tuzo ya heshima (wanawake)
Hope Powell ni mwana mama ambaye anamchango mkubwa Sana katika timu za wanawake nchini Uingereza baada ya kuwa kocha katika timu ya Taifa ya wanawake Uingereza akiwa na umri mdogo mwaka 1998 na pia tuzo hii imeenda kwake kutoka na mchango wake alioutoa katika timu ya wanawake ya Brighton and Hove Albion Kama kocha mkuu.
Leave your comment