Nyimbo Mpya: Harmonize 'Deka', Mac Voice 'Mama Yoyoo' na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Utashi na hari ya wasanii watanzania kutoa ngoma mpya kila siku ni moja ya vitu vichache ambavyo vinachagiza Bongo Fleva izidi kupasua mawimbi kila siku. Kama ulikuwa unatafuta makala ambayo itakusaidia kuvumbua hazina mpya za Bongo Fleva ambazo zitaweza kutajirisha maktaba yako ya muziki basi makala hii ni kwa ajili yako.

Soma pia: Washindi Tuzo za PFA 2021/22

Zifuatazo ni ngoma tano mpya na kali  kutoka Tanzania ambazo zimeingia sokoni wiki hii:

Deka - Harmonize

Kama uliweza kurahani Utamu Remix ya Harmonize na Mabantu basi bila shaka pia utaipenda "Deka" ngoma ya Harmonize ambayo ndani yake Harmonize na Mabantu wanaonesha ni kwa namna gani wanatumia pesa na mali walizonazo ili kunasa na kuwashawishi wanawake kimapenzi.

https://youtu.be/RAsfgRc_paI

Atakuoa Nani - Nay Wa Mitego, Stamina & Mabantu

Kwenye ngoma hii Nay Wa Mitego haoni haya kuwakumbusha wanawake hasa mabinti wadogo kujitunza na kuacha vitendo vya ujana kama starehe na anasa. Kwenye ngoma hii Nay Wa Mitego na Stamina wametumia maneno makali na ya kuudhi ili kuweza kufikisha ujumbe wao kwa mabinti.

https://youtu.be/QnQBHfd_X3E

Sir God - Baddest 47

Linapokuja suala la ubunifu na kujaribu midundo mipya basi msanii Baddest 47 huwa hana mpinzani na hili limedhihirishwa kwenye ngoma yake moya kuitwa "Sir God" ambayo ndani yake Baddest 47 anaomba Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu huku akitumia vionjo vya muziki wa Injili kufikisha ujumbe wake.

https://youtu.be/Kmf6P6kQ-oU

Mac Voice - Mama Yoyoo

Kutoka Next Level Music mwanamuzik Mac Voice ameachia bidhaa mpya kabisa ya kuitwa Mama Yoyo. Huu ni mkwaju ambao Mac Voice anamsifia mwanamke wake na kumuomba aweze kumfanya mke kabisa wa maisha. Ngoma hii imetayarishwa na Sound Bwoy kutoka Next Level na tayari imepokelewa vyema na mashabiki.

https://youtu.be/sI0-G1wwIWQ

Namwachia - Maua Sama

Wiki hii Maua Sama aliachia ngoma yake ya kuitwa na Namwachia ambayo ndani yake anaonesha kukatia tamaa mahusiano yake. Ngoma hii imetayarishwa na Yogo Beatz huku video yake ambayo imetayarishwa jijini Dar Es Salaam Tanzania ikiwa ni moja kati ya video chache kutoka Tanzania ambazo zimejaa ubunifu mkubwa.

https://youtu.be/hfaugFoIH_o

Leave your comment