Nyimbo Mpya: Diamond 'Oka', Nay wa Mitego 'Atakuoa Nani' na Ngoma Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii
10 June 2022
[Picha: Pulse Live]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo
Mashabiki wa muziki wa Tanzania wameendelea kupokea dozi nzito ya burudani kutoka kwa wasanii wao pendwa. Mtandao wa YouTube umekuwa mstari wa mbele kabisa kufanikisha hilo ambapo baadhi ya nyimbo kutoka kwa wasanii wa Tanzania zimefanya vizuri sana kwenye mtandao huo. Zifuatazo ni ngoma 5 kutoka kwa wasanii wa Tanzania ambazo zimefanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa wiki hii:
Soma Pia: Zuchu Atangaza Kuachia Nyimbo Mbili Mwezi Juni
Oka - Diamond Platnumz ft Mbosso
Video ya Oka ya Diamond Platnumz akimshirikisha Mbosso imeonekana kukosha macho ya mashabiki wengi wa muziki nchini Tanzania. Ukiweka kando mandhari na muktadha wa kiafrika uliopo kwenye video hii, bila shaka mitindo ya kucheza ya Mbosso na Diamond Platnumz imechagiza wengi kuvutiwa na video hii.
I Miss You - Rayvanny ft Zuchu
Kwa mujibu wa Director Ivan, video ya 'I Miss You' imetumia takriban Milioni 80 za kitanzania kuitengeza. Video hii inadhihirisha namna Rayvanny alivyokuwa na uchungu na hasira ya kuupeleka mbele muziki wa Bongo Fleva. Kufikia sasa, video hii imeshatazamwa mara Milioni 3.2 kwenye mtandao wa YouTube.
Badman - Tundaman Ft Harmonize
Video ya Badman ni ushahidi tosha kuwa Tundaman na Harmonize wana ubunifu ulioshiba. Pamoja na kuachiwa wiki mbili zilizopita, ngoma hii imeshatazamwa mara Milioni 2.2 kwenye mtandao wa YouTube.
La La - Mimi Mars ft Marioo
La La ni moja kati ya video kwenye kiwanda cha Bongo Fleva ambayo imejaa ubunifu wa kutosha. Kwenye audio, muingiliano mzuri wa sauti pamoja kati ya Mimi Mars na Marioo umefanya ngoma hii kuwa chaguo la kwanza masikioni mwa wasikilizaji. Kufikia sasa ngoma hii imeshatazamwa mara laki tano sitini na tatu huko YouTube.
Atakuoa Nani - Nay Wa Mitego ft Stamina & Mabantu
Huu ni wimbo ambao Nay Wa Mitego akishirikiana na Stamina na Mabantu wanahoji na kuwapa maarifa mabinti wadogo ambao wanapenda sana starehe wakitoa angalizo la moja kwa moja kuwa wajitunze na kujithamini ili wasikose kuolewa hapo baadae.
Leave your comment