Zuchu Atangaza Kuachia Nyimbo Mbili Mwezi Juni

[Picha: Rick Media]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki nyota kutokea lebo ya WCB Zuchu ametangaza kuwa anatarajia kuachia ngoma mbili mpya ifikapo Juni 24 mwaka huu. 

Soma Pia: Konde Music Worldwide Yafichua Sababu ya Kumuweka Kajala Kuwa Meneja wa Harmonize

Zuchu ambaye kwa mwaka huu ameachia ngoma moja tu, alitoa taarifa hizo kwa mashabiki zake kupitia akaunti yake ya Instagram, ambapo alisema kuwa tayari ameshawasiliana na Sallam SK ambaye amemruhusu kuachia ngoma mbili ya kwanza inaitwa 'Jaro' huku ngoma ya pili akiwaachia mashabiki zake waweze kuotea jina la wimbo huo. 

Aidha katika chapisho lake la Instagram,  Zuchu alidokeza kuwa nyimbo hizo mbili anataka kuziachia kama "project" au kazi rasmi ya kimuziki, ambapo msanii huyo aliwaomba mashabiki zake wamsaidie jina la "project", hiyo ambayo itasheheni nyimbo hizo mbili mpya. 

Ikumbukwe kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kwa Zuchu kuachia ngoma mbili kwa wakati mmoja kwani Septemba 13, mwaka 2020 miezi mitano tangu kutambulishwa kwake, Zuchu aliachia ngoma mbili ndani ya siku moja ambazo ni Cheche pamoja na Litawachoma, ngoma ambazo alimshirikisha Diamond Platnumz na mradi huo wa muziki aliupa jina la 'Side To Side'. 

Ndani ya mwaka huu, Zuchu ameachia ngoma moja tu ya kuitwa 'Mwambieni' ambayo iliachiwa mwezi Januari. Kufikia sasa, mgoma hio imefanya maajabu makubwa huko YouTube kwani imeshatazamwa zaidi ya mara Milioni 10. 'Mwambieni'  ni moja kati ya video za mwaka 2022 ambazo zimetazamwa sana kwenye mtandao wa YouTube kutoka kwa msanii wa Tanzania. 

Leave your comment