Nyimbo Mpya: Rayvanny ft Zuchu 'I Miss You' na Ngoma Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mtandao wa YouTube umekuwa ni kipimo cha watu kuweza kufahamu iwapo ngoma imefanya vizuri. Pia kupitia mtandao huo, mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva wanapata nafasi ya kutazama video na kusikiliza muziki kwa wasanii wao wanaowapenda. 
Zifuatazo ni ngoma tano ambazo zinafanya vizuri sana Tanzania kwa wiki hii: 

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rich Mavoko 'Blow Up', Fid Q 'Kiberiti' na Ngoma Zingine Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

I Miss You - Rayvanny Ft Zuchu
Video ya ngoma hii itahesabika kama moja ya video bora kuwahi kutengenezwa kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva Rayvanny amekiri kuwa alitumia takriban Milioni 15 katika kile kipande cha video ambacho alichoma nyumba. Kufikia sasa video hio imeshatazamwa mara Milioni 1.7 kwenye mtandao wa YouTube. 

https://youtu.be/EYfwcskpCis

Badman - Tundaman ft Harmonize
Hii ni ngoma ambayo kwa sasa inatamba sana nchini Tanzania na inasikika sehemu mbalimbali. Ukiweka kando mashshiri mazuri, midondoko ya kusisimua  pamoja na muingiliano mzuri wa sauti, video ya ngoma hii ambayo ni ya tofauti na imejaa ubunifu wa hali ya juu imefanya kazi hii kuwa ya kipekee. 

https://youtu.be/RS9PMaKJHQ4

Kioo - Anjella ft Harmonize
Video ya Kioo hatimaye imefika sokoni na bila shaka mashabiki wameipokea kwa mikono miwili ikiwa ni video ya nne ambayo imewakutanisha CEO na First Lady wa Konde Gang yaani Anjella na Harmonize. Kufikia sasa ngoma hii imetazamwa mara Milioni 1.2 kwenye mtandao wa YouTube. 

https://youtu.be/gd5CMNZc8JM

La La - Mimi Mars ft Marioo
Director Kenny kwa mara nyingine ameonesha ufundi wake katika kuandaa video nzuri hasa kupitia video ya La La ya kwake Mimi Mars akiwa amemshirikisha Marioo. Hii ni video ya kwanza kutoka kwa Mimi Mars tangu kuanza kwa 2022 na kufikia sasa imeshatazamwa mara nne arobaini na tano kwenye mtandao wa YouTube. 

https://youtu.be/S4mcZTt2EY4

Sugar Remix - Jay Melody Ft Marioo 
Ngoma ya Sugar Remix imeendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube na kufikia muda huu, kazi hii ya Jay Melody akiwa amemshirikisha Marioo tayari imepata kutazamwa mara laki tisa sitini na nane huko YouTube. 

https://youtu.be/XojdvTGoj7s

Leave your comment