Ushindi wa Mohamed Salah Mchezaji Bora wa mwaka -PFA fans'

[Picha: football-espana.net]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Nahodha wa timu ya Taifa ya Misri na winga wa timu ya Liverpool Mohamed Salah ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa kampeni ya Ligi Kuu kwa mwaka 2021/22 inayotolewa na Chama Cha wachezaji mpira wa kulipwa Professional Footballer Association (PFA)

Ikiwa ni Mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo baada kushinda katika msimu wa mwaka 2017/18, kinara huyu wa magoli katika Ligi ya Uingereza ameweza kuisaidia Liverpool kunyakua ubingwa wa Carabao Cup pamoja FA Cup kwa msimu huu na pia katika Ligi ya mabingwa Ulaya ameweza kuisaidia Liver kufika fainali na kushindwa kunoa dafu mbele ya Real Madrid.

Soma Pia: Historia Fupi ya Jose Mourhino Katika Soka "The Special One"

Kwa timu ya Taifa pia Salah ameweza kufika fainali akiwa na timu yake ya Taifa ya Misri kwa mwaka huu Ila wakashindwa kutunisha misuli mbele ya Senegal, timu ambayo Sadio Mane mchezaji mweza wa Liverpool anaichezea.

Salah katika msimu huu Huko Uingereza ameweza kushinda kiatu Cha dhahabu baada ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi zaidi akiwa sawa na Son Heung Min winga wa Tottenham Hotspurs katika msimu huu ambapo Salah amekuwa na jumla ya magoli 31 katika michuano yote na pasi 16 za usaidizi wa magoli katika michuano yote.

Katika tuzo hizo zilizotolewa hivi karibuni Mohamed Salah alikuwa akishindanishwa na wachezaji mbalimbali Kama vile mchezaji mwenza wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, Kevin De Bruyne, Phil Foden, Declan Rice, pamoja na Conor Gallagher katika tuzo hizo.

Leave your comment