Harmonize 'Dunia', Marioo 'Naogopa' na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Imekuwa ni wiki yenye pilkapilka nyingi sana kwenye kiwanda cha Bongo Fleva kutokana na wasanii wengi kutoa nyimbo kali, ambazo mara zote zimekuwa zikishindana kuhusu ipi itakaa juu zaidi kwenye chati za muziki ikiwemo kwenye mtandao wa YouTube.

Bila shaka kama unafuatilia muziki kutoka Tanzania utakuwa na hamu ya kufahamu ni ngoma gani ambazo zinasikilizwa sana YouTube Tanzania kwa wiki hii. Zifuatazo ni ngoma tano ambazo zinatamba na kufanya vizuri sana nchini Tanzania kwa wiki hii.

Naogopa - Marioo ft Harmonize

Mashabiki wamezidi kuipaisha ngoma ya Marioo ya Naogopa ambayo amemshirikisha Harmonize. Mashahiri mazuri, muingiliano mzuri wa sauti pamoja na ubunifu mkubwa katika video ni baadhi ya vitu ambavyo vimevutia watazamaji kuweza kuendelea kupenda kazi hii.

https://www.youtube.com/watch?v=LJONP5YAokU

Dunia - Harmonize

Harmonize ameendelea kuimarisha ufalme wake huko YouTube kupitia video ya Dunia ambayo imeachiwa siku takriban 12 zilizopita. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2.8 kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni video ya tano kutoka kwa Harmonize kwa mwaka 2022.

https://www.youtube.com/watch?v=yKJVlADjpus

Soma Pia: Marioo ft Harmonize ‘Naogopa’, Diamond ‘Wonder’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii

Sugar Remix - Jay Melody ft Marioo

Ukiweka kando ubora wa ngoma hii pia video ya 'Sugar Remix' imevuta umakini mkubwa wa watazamaji na ndio maana ndani ya siku tatu tu tangu kuachiwa kwake, tayari ngoma hii imepata umaarufu mkubwa na  imeshatazamwa mara laki tatu sabini na nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=XojdvTGoj7s

Sona - Diamond Platnumz ft Adekunle Gold

Video ya Sona ni zawadi nyingine ya Diamond Platnumz kwa mashabiki zake kutoka kwenye EP yake ya kuitwa First Of All. Takriban wiki mbili zimeshakatika tangu Diamond Platnumz aachie video ya Sona ambayo imeongozwa na TG Omori l. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.8 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=zpSj2Z2tbOg

Kioo - Anjella ft Harmonize

Ngoma ya Kioo imezidi kuthibitisha kuwa Anjella na Harmonize wana "chemistry" nzuri pale ambapo wawili hao husjirikiana pamoja. Sanaa ya kucheza na maneno pamoja na mashairi shirikishi yamepelekea ngoma hii kupendwa sana. Mpaka sasa imeshatazamwa mara laki nne ishirini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=8zTFf-dwz5I

Leave your comment