Anjella ‘Kioo’, Yamoto Band ‘Mjini Kuna Mambo’ Na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Imekuwa ni wiki nzuri sana kwenye uwanja wa muziki wa Bongo Fleva baada ya mashabiki kuweza kuburudishwa na ngoma kali ambazo wasanii kutokea Tanzania wamekuwa wakiziachia sokoni ndani ya wiki hii. Zifuatazo ni ngoma kali ambazo zimeachiwa na wasanii wa Tanzania kwa wiki hii:

Soma Pia: Marioo ft Harmonize ‘Naogopa’, Diamond ‘Wonder’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba Bongo Wiki Hii

Kioo - Anjella ft Harmonize

Baada ya kuachia Toroka mwanzoni mwa mwaka huu, wiki hii Anjella alichangamsha Bongo Fleva na ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Kioo ambayo amemshirikisha Harmonize. Hii ni ngoma ya mapenzi ambapo Harmonize na Anjella wanasheherekea mambo mazuri ambayo wapenzi wanatakiwa kufanyiana.

https://www.youtube.com/watch?v=8zTFf-dwz5I

Niteke (Video) - Alikiba ft Blaq Diamond

Wiki hii Alikiba aliachia video ya ngoma yake ya Niteke akiwa na kundi la Blaq Diamond. Bila shaka hii ni moja kati ya video bora kutoka kwa Alikiba kwani imepambwa na mitindo mizuri ya kucheza pamoja na ubunifu mkubwa.

https://www.youtube.com/watch?v=l696Po6vjwo

Sugar Remix - Jay Melody ft Marioo 

Itoshe kusema hii ni moja ya collabo ambayo imeweka alama kubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva. Muingiliano mzuri wa sauti, ushirikiano kati ya wasanii hawa pamoja na midondoko ya ngoma hii umepelekea wimbo huu ambao pamoja na kwamba hauna video, kuweza kutikisa na kusikika kila kona ya Tanzania.

 https://www.youtube.com/watch?v=BBPe8fyAffM

Mjini Kuna Mambo - Yamoto Band

Kundi la Yamoto Band limeendelea kukoleza burudani kwa wapenzi wa muziki kupitia ngoma yao mpya a’Mjini Kuna Mambo’, ambayo inatoa angalizo kwa wanawake wanaoishi kijijini kuweza kuwa makini pale wanapotaka kwenda kuishi mjini. Mjini kuna mambo imesindikizwa na video kali yenye stori ya kuvutia.

https://www.youtube.com/watch?v=NShzI7_JaOw

Doreen - Lody Music

Huu ni wimbo makhususi ambao wanaume wanaweza wakatumia kufurahisha wenza wao. Kwenye Doreen, Lody Music anamwaga sifa kedekede kwa msichana anayeitwa Doreen kutokana na urembo pamoja na tabia njema ya mwanadada huyo.

https://www.youtube.com/watch?v=0_1tsvl33LY

Messiah - Walter Chilambo

Walter Chilambo anazidi kusongesha mbele gurudumu la muziki wa Injili kupitia ngoma yake mpya ya Messiah ambayo ndani yake anaeleza ukuu na utukufu wa Mungu na namna gani Mungu ni muweza katika maisha ya kila siku.

https://www.youtube.com/watch?v=xCtE627xaFE

Leave your comment