Ubashiri Mechi ya Manchester United Vs Norwich City Jumamosi hii

[Picha: skysports.com]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Katika kuelekea mzunguko wa 32 kati ya 38, sasa mashetani wekundu Manchester United wanaenda kuvaana na Norwich City Jumamosi hii kwenye hatua za mwisho mwisho za msimu wa Ligi kuu ya EPL.

Norwich ambao kwa sasa ndio wanaoshika mkia huko EPL wanakaribishwa na United katika uwanja wa Old Traford huko jijini Manchester ikiwa ni katika hatua za kupata alama tatu muhimu ili waweze kubaki katika kuu ligi hiyo.

Baada ya mizunguko 31 kupita kwa timu zote mbili, sasa United tayari wana alama 51 wakiwa nafasi ya 7, huku wao Norwich wakishika mkiwa katika nafasi ya 20 wakiwa na alama 21 tu.

Mechi hii itakuwa mechi ya muhimu sana kwa timu zote kwani  Norwich kushinda mechi hiyo itawapandisha nafasi moja zaidi lakini kushinda mechi hii haiwahakikishii kutokushuka daraja.

Kwa wao United pia magoli zaidi pamoja na ushindi ni muhimu sana kwao  kwani kwa nafasi ya 7  aliyopo United nyuma ya Tottenham Hotspurs walio nafasi ya 4 kwa tofauti ya alama 6, inamfanya ashindwe kushiriki katika mashindano yoyote makubwa ikiwemo UEFA Champions League pamoja na Europa league.

Kwa upande wa majeruhi Manchester United wao watawakosa wachezaji kama Fred, Luke Shaw, Scott Mctominay, Edinson Cavan, Raphaël Varane pamoja na Greenwood ambaye pia asimamishwa kushiriki mechi za United.

Nao Norwich majeruhi wao ni Adam Idah, Joshua Sargent, Ozan Kabak, Andrew.

Soma pia: Tetesi za Lewandowski kuhamia Barcelona

katika michezo 12 ambayo Norwich na United walishakutana huko nyuma ni mechi 2 tu Norwich alichomoa kwa United na mechi 10 United alishinda na hakuna droo Kati yao.

Kwa kumbukumbu hizi na kwa nafasi aliyopo Norwich katika ligi United wanaonekana kuwa na nafasi nzuri licha ya kuwa mpira wa miguu unamatokeo yoyote hivyo kwa timu zote mbili kufunga odds za 1.91 zimetolewa

Leave your comment