‘Jeshi’, ‘Teacher’ na Nyimbo Zingine za Harmonize Alizogusia Maisha Yake Binafsi

[Picha: NME]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Ali Kiba Bila Malipo Kwenye Mdundo

Tangu aanze muziki kwenye lebo ya WCB mwaka 2015, Harmonize amekuwa ni moja ya wasanii bora sana kuwahi kutokea kwenye historia ya Bongo Fleva. Moja ya silaha ambayo imeweza kumfikisha hapo ni pamoja na uandishi bora wa nyimbo zake. Harmonize ni moja ya wasanii wachache duniani ambao wanaweza kuelezea mambo yao binafsi ya kimaisha kwenye nyimbo zao.

Pakua Nyimbo za Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mara zote Harmonize huwa hafanyi ajizi kuzungumzia mahusiano yake ya kimapenzi, washindani wake wa kimuziki, bifu na hata kutaja majina ya baadhi ya watu wake wa karibu kwenye nyimbo zake, zote hizi zikiwa ni harakati za kuwajulisha mashabiki zake nini hasa kinaendelea kwenye maisha yake ya kila siku. Zifuatazo ni ngoma tano kutoka kwa Harmonize ambazo amegusia maisha yake binafsi:

Vibaya

Huu ni wimbo ambao Harmonize aliuachia makhususi kwa ajili ya mpenzi wake za zamani wa kuitwa Kajala Masanja. Hii ni ngoma ambayo iliashiria kuwa mahusiano yake na Kajala Masanja yamefikia mwisho kwani kupitia mistari ya ngoma hii, Harmonize anamkumbusha Kajala viapo vya kimapenzi ambavyo waliwekeana na kumuomba wasichukiane na kusemana ‘Vibaya’ hata wakiachana.  Kwenye aya ya kwanza ya ngoma hii Harmonize anaimba : "Sitaki kuamini kwamba lile kapu la mabaya yangu halina hata machache mema. Nitakuwa mshamba nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu ili nionekane mwema. Japo mapenzi yanaumiza I wish tusisemane Vibaya"

https://www.youtube.com/watch?v=zEtsp8BlyM4

Jeshi

Jeshi ni wimbo ambao ulimtambulisha rasmi Harmonize nje ya lebo yake ya zamani ya kuitwa WCB. Huu ni wimbo ambao Harmonize anajipongeza kwa mafanikio aliyoyapata na ukubwa alionao na ndio maana anastahili kuitwa Jeshi. "Kamwe Siwezi kujibizana ila mwenzenu nimeumbwa na subra, cheki madili yanavyogongana coz nyota yangu ni Libra," anaimba Harmonize kwenye aya ya pili. Aidha kwenye ngoma hii, Harmonize anatoa shukrani za dhati kwa mashabiki zake wote hasa jamii ya mitandaoni kuanzia Twitter na Instagram kwa kumshika mkono huku akipeleka shukrani za dhati kwa Master Jay na Madam Rita kwa kumpa moyo wa kupambana kwenye muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=EWkzKrzeMdA

Never Give Up

Huu ni wimbo ambao Harmonize ameweza kuhadithia historia yake ya kimaisha tangu alipotoka huko Mtwara, kukutana na Diamond Platnumz mpaka kuanzisha kiwanda chake cha kuchakata vipaji vipya cha kuitwa Konde Music Worldwide. Harmonize anawaaminisha watanzania kwenye wimbo huu kuwa yeye ni maana halisi ya kutokukata tamaa. "Najua maisha safari na bado sijafika I got long way to go ila naona afadhali kulala uhakika na kula so ka before," anaimba Harmonize kwenye aya pili ya ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=IrPrf3cSmrg

Teacher

Teacher ni ngoma ambayo ndani yake Harmonize ameonesha ukubwa wake, namna ambavyo amebadilisha kiwanda cha muziki Tanzania na jinsi gani wasanii wengine wakubwa wanafuata nyendo zake ikiwemo kuiga aina yake ya muziki. "Wakati wanahanya kugombea kiti, wanadanganyana na viewers wa kucheat mie jicho liko nyanya nishakula kijiti na magoma yakipigwa huko club mtiti," anaimba Harmonize mwanzoni kabisa mwa Amapiano hii.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Mtaje

Kama ambavyo Diamond Platnumz alimsifia Wema Sepetu kwenye ‘Moyo Wangu’ au Rayvanny alivyoandika ‘Valentine’ maalum kwa ajili ya mpenzi wake Paula Kajala, basi Harmonize alifuata kwa kuandika wimbo wa ‘Mtaje’ kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja. Mtaje ni ngoma ambayo Harmonize amejimaliza kwa Kajala kwa kumpa sifa kedekede mpenzi wake huyo bila kumtaja jina na mwishoni kabisa ya wimbo huu Harmonize anawapa ‘homewor’ mashabiki zake kuwa wawaulize watu wake wake wa karibu kama Jose Wa Mipango, Alice Kella na Uncle Duke maana wanajua ni nani hasa ameimbiwa wimbo huo.

"Ana kasura kaupole miaka nenda rudi hazeeki tena ni mtu wa gym gym, shepu ndo linanipa wazim wazim na tattoo nimchore ila ndo hivyo tena hapendeki ama kweli mapenzi hayana mwalimu, wengine hata kuniona ni adimu" anaimba Teacher mwanzoni kabisa mwa ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=UbqLboruK8M

Leave your comment