Rich Mavoko ‘Fundi’ Album, Nandy ‘Siwezi’ na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Nyimbo za Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Ni wiki nyingine tena ambayo wasanii wa Bongo Fleva wameendelea kushusha burudani kwa mashabiki zao kwa kuachia ngoma mpya ambazo zina lengo la kuchangamsha kiwanda cha muziki. Zifuatazo ni ngoma tano mpya ambazo, zimeachiwa wiki hii kutoka Tanzania:

Pakua Nyimba zake Rosa Ree Kwenye Mdundo Bila Malipo

Siwezi - Nandy 

Wiki hii mwanamuziki Nandy aliachia ngoma yake mpya ya kuitwa Siwezi ambayo ndani yake anaonesha jinsi mapenzi yanavyomuumiza na kuumiza hisia zake. Video ya ngoma hii ambayo imejengwa na stori nzuri ya kusikitisha imezidi kunogesha kazi hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.3 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=FuK_yKDdmHo

Fundi (Albamu) - Rich Mavoko

Rich Mavoko alitetemesha kiwanda cha muziki wiki hii baada ya kuachia albamu yake Fundi ambayo imesheheni ngoma 16 akishirikisha wasanii nyota kutoka Tanzania kama Fid Q na Sarafina pamoja na Ssaru, Nviiri The Story Teller na H_art The Band kutokea nchini Kenya. Hii ni albamu ya kwanza kutoka kwa Rich Mavoko ikiwa imetoka mwaka mmoja tangu aachie Mini Tape yake mwaka 2020.

https://www.youtube.com/watch?v=D_Ib7OtfzOI

Soma Pia: Diamond ‘Fine’, Nandy ‘Siwezi’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania

Yeeh - Moni Centrozone ft Marioo

Kibao hiki cha Yeeh kimenogeshwa hasa na michano mikali ya Moni Centrozone pamoja na sauti makini ya Marioo ambayo inasikika zaidi kwenye kiitikio. Ufundi wa Hanscana katika kuandaa video kali umeonekana zaidi kwenye video ya wimbo huu ambao ndani ya muda mfupi tangu kuachiwa kwake umepata mafanikio makubwa kwenye mitandao mbalimbali ya kuuza muziki.

 https://www.youtube.com/watch?v=jISRfdmmraQ

Freestyle Session 4 - Young Lunya

Itoshe kusema kuwa Young Lunya ni moja kati ya wana Hip-Hop ambao wana uwezo mkubwa wa kuandika mistari ya kujitamba na kujipa sifa yeye binafsi. Freestyle Session 4 imekuja kipindi ambacho kulikuwa na uhaba wa ngoma kali za Hip Hop kwenye muziki wa Tanzania na bila shaka ngoma hii imeweza kufanya vizuri sana kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Themanini na Tatu Elfu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=N7fPapsMH_s

Blue Print - Rosa Ree

Kwenye Blue Print, Rosa Ree anasheherekea historia ya Afrika. Kwenye ngoma hii Rosa Ree anaeleza jinsi ambavyo utamaduni wa mwafrika umekuwa ukiathiriwa na wazungu huku video ya ngoma hiyo ikisindikiza mashahiri ya kazi hiyo kwa kuakisi kile kilichoibwa kwenye mashahiri.

https://www.youtube.com/watch?v=g15QiRwyu7g

Leave your comment